Hawa ndio viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome. Kutoka kushoto ni Mjumbe Bakari Hizza, Diana Olotu
(Katibu msaidizi) Andrew Chole Mhella( Katibu)Leonce Uwandameno (mwenyekiti), Awadhi Suleiman
(Mweka hazina)na mwisho ni Erasmus Luhoyo (Mwenyekiti msaidizi)
Wakina mama nao walikuwa wakifurahia siku hii maalum kwa Jumuiya.
Kwanza kabisa, kwenye kipindi cha mwaka uliopita, Jumuiya ya Watanzania Rome imefanikiwa kuitangaza Tanzania kwa wenyeji wetu hapa Italia. Mafanikio ya kuitangaza Tanzania yalitokana na mikakati kadhaa kama vile jumuiya ilipoandaa SIKU YA UTAMADUNI WA TANZANIA.
Tatu, Jumuiya pia inafuraha kuwajulisha pia kwenye mwaka ulioisha imefanikiwa pia kufungua Account ambapo kwa wale ambao hawataweza kufikisha michango yao kwa mweka hazina wanaweza kudeposit michago moja kwa moja kwenye account ya Jumuiya.
Katika mkutano wa jana pia kulikuwa kuwe na uchaguzi mkuu wa viongozi wapya kwa mujibu wa katiba. Lakini kutokana na wanajumuiya hai kutofikia idadi inayotakiwa kikatiba, uchaguzi uliahirishwa mpaka hapo itakapotamgazwa tena. Kwa maelezo zaidi na picha tafadhali tutembele hapa, www.watanzania-rome.blogspot.com.
Andrew Chole Mhella,