Read Time:34 Second
Jumuiya ya watanzania ugiriki ilisherehekea miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye ofisi ya jumuiya J’mosi 14/02.Tulilazimika kuichelewesha kwa siku mbili kutokana na mihangaiko ya kikazi.
WABONGO UGHAIBUNI
Sherehe zilianza kwa wimbo wa Taifa na kufuatiwa na risala fupi ya Mwenyekiti mwanzilishi wa Jumuiya yetu bw.Suleiman Nassib (DIDOS)ambae alisisitizia umuhimu wa umoja na ushirikiano.
Ilifuatiwa na shukurani za bi.Joan mwakilishi wa kikundi cha wanafunzi wa Holland tuliowakaribisha rasmi katika sherehe yetu.
Baadae mke wa Mwenyekiti Bi Asha Chunda alikata keki maalum ya mapinduzi na bw.Jackson na bi Sandra walitumbuiza na kuchangamsha ukumbi kwa nyimbo zao zilizowanyanyua hata wageni wetu.
Sherehe ziliendelea hadi alfajiri
KAYU LIGOPORA
KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI
Dodoma TANZANIA Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura 369 baada ya kuteuliwa…
01/11/2025 ‘Uchaguzi umeisha tusimame pamoja kama Taifa’ – Hotuba ya Kwanza ya Samia Suluhu Rais Samia Suluhu Hassan akabidhiwa cheti cha ushindi wa uchaguzi wa 2025 na Tume Huru ya…

















