Balozi wa Tanzania nchini Afrka Kusini Meja Jen (Mst) Gaudence Milanzi tarehe 25 May 2020 alisimamia zoezi la repatriation (usafirishaji) wa dharura) ya Watanzania na raia kadhaa wa nchi hiyo waliokwama kutokana na Lockdown na kusitishwa safari za ndege, kutoka Johannesburg kuja Dar
Taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini humo zinasema kwamba Balozi Milanzi aliratibu na kusimamia zoezi hilo ambapo Watanzania 14 ambao walikwama nchini humo kwa miezi miwili kufuatia Lockdown hiyo.
Raia 12 wa Afrika Kusini pamoja nna raia mmjoa wa Uingereza nao wakajiunga kwenya msafara huo baada ya kuona ni afadhali warejee Tanzania ambako hakuna Lockdown ili kuendelea kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo.
Raia 12 wa Afrika Kusini pamoja nna raia mmoja wa Uingereza nao wakajiunga kwenya msafara huo baada ya kuona ni afadhali warejee Tanzania ambako hakuna Lockdown ili kuendelea kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo.
Akiwasindikiza abiria hao walioondoka kwa ndege ya kukodi ya kampuni ya AS SALAAM AIR ya Zanzibar, Balozi Milanzi aliwapa pole kwa kuwa katika Lockdown ya miezi miwili na kuwatakia safari njema na maisha ya furaha watapowasili
Tanzania ambayo ni nchi pekee ambayo imekuwa na msimamo thabiti wa kupambana na gonjwa la COVID 19 lililosababisha nchi zingine kufungia kila mtu ndani.