
WANGI YI AWASILI NCHINI, KUZINDUA VETA
Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi ameanza ziara yake ya kikazi ya kikazi nchini Tanzania.
Mhe. Wangi Yi amewasili majira ya saa 11 jioni katika uwanja wa ndege wa Geita – Chato na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb).
Mara baada ya kuwasili, Mhe. Wang Yi ameshiriki katika uzinduzi wa chuo cha Veta kilichopo Chato mkoani Geita, ambapo ujenzi wa chuo hicho umegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza wakati akimkaribisha Mhe. Wang Yi katika uzinduzi wa chuo hicho, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka umuhimu mkubwa katika Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ili kufanikisha kujenga uchumi wa viwanda, na kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.