0 0
Read Time:57 Second

Mhe Neema Lugangira (Mb.) aliandaa Mkutano “Tanzania Maternal Mortality and Nutrition – Mama Mjamzito na Mbogamboga” uliolenga kujadiliana kuhusu uhusiano kati ya vifo vya upwakina mama wanapojifungua na lishe kwa maana ya upungufu wa damu. Zaidi ya watu 50 walishiriki kupitia Mtandao wa Zoom.

Watoa mada waliwakilisha makundi muhimu kama ifuatavyo:

  1. Dr. Grace Moshi – Msimamizi wa Masuala ya Lishe; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
  2. Dr. Lilian Mnabwiru – Katibu; Chama Cha Madaktari Tanzania
  3. Anna Sengoka; Chama Cha Wakunga Tanzania
  4. Dr. Ali Said – Daktari Bingwa wa Masuala ya Wanawake na Mwalimu MUHIMBILI
  5. Dr. Isihaka Mwandalima – Mkurugenzi (Technical) – Shirika lisilo la Kiserikali (NGO); Pathfinder International

Mkutano huu uliendeshwa na Wenyeviti Wawili; Mhe Neema Lugangira (Mb.) na Dr. Frank Minja; Rais wa Diaspora ya Watanzania wanaoishi Marekani.

Baada ya Mkutano, Mbunge Neema Lugangira alisema “ni dhahiri Mkutano huu wa kwanza ambao kwa hakika umedhihirisha umuhimu wa lishe bora kwa mama mjamzito kabla, wakati na baada ya kujifungua. Hivyo, ni dhamira yangu kuendelea kuandaa mijadala ya namna hii kwa njia mbalimbali”.

Kama hukubahatika kushiriki katika majadiliano haya LIVE unaweza kusikiliza mjadala mzima uliorekodiwa kupitia link hii na ukasoma chat nzima kupitia link hii

Karibuni Sana.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %