
Na Dr Yahya Msangi

Unafiki ni hulka sawa na kusengenya. Msengenyaji huogopa kusengenya ikiwa anayemsengenya yupo karibu na alipo! Husubiri mhusika aondoke au yéyé mwenyewe msengezaji huenda mbali ili aweze kusengenya.
Magufuli hakuwa malaika. Alikuwa binadamu “fallible” kama binadamu mwingine yeyote. Lakini wanafiki ambao wengi aliwakweza yéyé mwenyewe wamesubiri ameondoka ndiyo wanaanza kumsengenya. Wameacha ya maana aliyotenda wameshupalia mapungufu yake. Hâta Mwalimu alipong’atuka baadae alikuja kuwauliza aliodhani walikuwa wanafunzi watiifu: vipi mmachame ya maana mnatukuza mambo yangu ya hovyo? Naamini hâta Magufuli angeamka leo angewauliza baadhi yetu swali hili hili!
Hakuna suala linawaanika kilingeni wanafiki kama suala la bandari. Utadhani katika uhai wake Magufuli alishughulika na Bandari tu! Na ni mmoja wa aliowakweza ndiye kageuza bandari ndio legacy aliyoacha Magufuli! Yéyé na wenzie wanasahau mambo ya msingi aliyosimamia Magufuli.
Hakika hakuna mambo yaliyotukwamisha kimaendeleo kama
- wizi wa mali ya umma,
- .ufisadi
- mikataba mbovu,
- nidhamu mbovu maofisini
- usimamiaji mbovu wa makusanyo na matumizi ya mapato.
Kwa kutambua haya Magufuli alitumia muda wake wote kuyapatia tiba. Wizi na ufisadi ulikithiri kiasi mtu kuwa mwaminifu alionekana mjinga. Semina, makongamano, mikutano ikawa ndio kazi kuu maofisini! Miradi haiishi kwa wakati na ikiisha viwango vya chini mnoo! Kwa muda wa miaka 5 tu Magufuli alikaribia kumaliza haya matatizo.
Nilitegemea waliojifanya kumpenda hivi sasa wangejikita kujadili namna ya kudumisha au kuboresha mbinu za Magufuli. Mbinu za Magufuli zimetambulika na UN! Magufuli katengewa “session” ndani ya UN kumjadili! Hatukuwahi kuona raisi aliyefia madarakani akijadiliwa kama Magufuli ndani ya makao makuu ya UN New York!
Kila aliyezungumza alieleza kufurahishwa kwake na mambo matatu: kufanikiwa kupungua ufisadi, kuipeleka nchi yake uchumi wa miaka 4 kabla ya ilivyotabiriwa na UNDP na kuboresha utendaji serikalini. Mnyonge mnyongeni lakini….!
Wakati UN na jumuia mbalimbali zikielezea mafanikio ya Magufuli chombo chetu kikuu cha kutunga sheria kimejikita kujadili bandari ya Bagamoyo!
Anayeongoza mjadala ni Spika! Kwa kuwa nafsi zinawasuta wanajifanya kukemea wanaomdhalilisha Magufuli! Wanasahau wao ndio wanaongoza kumdhalilisha? Bunge letu limeshindwa hâta kutoa AZIMIO kuishauri au kuitaka serikali iwasilishe mpango wa jinsi itakavyoendeleza, kuboresha na kuyalinda mazuri yote yaliyotendwa na Magufuli ! Serikali ituambie ni vipi itaendelea kukusanya mapato n’a kuyatumia, nidhamu maofisini, kutufikisha uchumi wa juu, kuendeleza ujenzi wa miundombinu, mashule, zahanati, n.k.








