0 0
Read Time:2 Minute, 34 Second

Na Dr Yahya Msangi

Nianze kwa kusema kuwa kifo cha binadamu yoyote hâta angekuwa mbaya kiasi gani hakipaswi kufurahiwa. Nimuombe Allah amsamahe makosa yake Idris Derbi.

Nimeona mtandaoni wachambuzi uchwara wakimsifu Derbi ambaye kauawa na wa Tourag na sio Boko Haram kama wengi wanavyodai.

Hadithi ya Boko Haram imepandikizwa na France ili kuficha ukweli wa kinachoendelea Tchad, Cameroun, Mali, Niger na Central Africa. Kote huko baadhi ya raia wameamua kupinga muendelezo wa ukoloni wa kifaransa nchini mwao. Nchini Tchad, Mali na Niger kabila la Tourag (wengi waislam) limeamua kupambana na ukoloni mamboleo ambao watu kama kina Derby, Bongo na wenzao wanatumika kupora utajiri wa mali asili. Hâta Tanzania Magufuli angeweza kuitwa Boko Haram kama angekuwa kwenye koloni la mfaransa maana alipinga uporaji mali asili za Tanzania.

Katika maeneo ya wa Tourag hasa nchini Mali na Tchad kuna utajiri mkubwa wa uranium ambao ndio unawatoa udenda wafaransa! Uchunguzi unaonyesha vinu vyote vya kuzalisha umeme wa nuklia nchini ufaransa vinategemea uranium ya Tchad na Mali. Ufaransa itashindwa kuwasha umeme ikiwa sa Tourag watafanikiwa kudhibiti uranium yao. Wala wa Tourag hawataki kuzuia uranium yao isitumike na wafaransa. Wanachodai ni ufaransa ilipe bei iliyoko sokoni na iwalipe fidia wa Tourag wote ambao Afya Zao zimeathirika kutokana na uchimbaji uranium wa hovyo ambao umeathiri afya zao, mifugo yao na mazingira. Vyanzo vyao vya maji vimekuwa n’a viwango vya juu mno vya uranium kiasi kwamba watu wamepata kansa kwa kiwango cha kutisha. France imekataa kukaa na watourag kwa kuwa watawala kama hujui Idris ni vibaraka wao. Ndipo sa Tourag walipoamua kuanzisha mapambano ya silaha ili kutwaa madaraka ya nchi au kujitenga na Tchad. Hawa ndio waliompiga shaba Idris ambaye kwa kiburi aliamini watourag ni watu wasio na nguvu na mara kadhaa amekuwa akienda vitani. Haraka baada ya kifo chake mara tu aliporudishwa Djamena kwa matibabu mkoloni kamchomoa mtoto wa Idris na kumpa madaraka ya babaake! Kwenye haya makoloni mamboleo mtoto kumrithi baba imekuwa kawaida! Mfaransa ndie anaamua nani awe mkuu wa nchi.

Aliyekuwa Rais wa TCHAD Idris Derbi.
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %