0 0
Read Time:1 Minute, 58 Second

George Michael Uledi.
Kyela, Mbeya.
April 21, 2021.

Kuna wakati CCM ilikuja na ahadi za mwana Tanu na ninadhani sasa wakati umefika wa kutengeneza na kuziimba amri kumi kwa Taifa langu. Hii inaweza kuwa moja ya alama kubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake! Nawaza kuwa labda katika kujenga Taifa lenye nidhamu na mshikamano tunapaswa kuwa na kitu cha namna hii;

  1. Nina imani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee na u
    utanzania wangu na kwamba tunaweza kuwa Taifa bora duniani tukifanya kazi kwa bidhii, maarifa, nidhamu na utii!
  2. Nitakuwa mfano wa kuigwa katika uadilifu na uzalendo kwa familia yangu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutimiza malengo ya pamoja ya Taifa kabla ya kutimiza malengo yangu binafsi.
  3. Nitachukia rushwa, ubinafsi, wizi, uzembe na kujitoa kutumikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia elimu yangu, maarifa yangu, imani yangu kwa maslahi ya Watanzania wa rika zote.
  4. Kila mara nitasisitiza na kuuishi umoja wa kitaifa, undugu na kuukataa ukabila, udini, ukanda, matabaka kwa lengo la kudumisha mshikamono katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  5. Nitajitoa kutetea maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka tone la mwisho la damu yangu kwa kulinda Uhuru wa mipaka ya Taifa, kulinda maslahi ya kiuchumi ya Tanzania pamoja na maslahi ya tamaduni za Tanzania.
  6. Sitathubutu kuisema vibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wake wa sasa na wastaafu kwa lengo la kulinda heshima na sura njema ya Taifa langu Tanzania.
  7. Nitafanya maombi kwa imani yangu kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wake kabla ya kufanya maombi yangu binafsi.
  8. Nitajitoa kwa kadri ya uwezo wangu na kila siku ntawaza ni kitu gani chema niifanyie Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake.
  9. Nitakuwa na heshima kwa watu wa rika zote na kulinda maadili, mila na tamaduni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, ukatiri kwa watoto na kulinda haki za walemavu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  10. Nitakuwa msemaji hodari wa mafanikio na maono ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania popote nitakapokuwa ndani na nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ntajitaidi kujivunia Nchi yangu katika viwango vya juu kabisa.

Mungu wangu nisaidie!

Ahadi hizi zitaendelea kupalilia na kukuza uzalendo wa raia wa Tanzania pamoja na kuimarisha umoja/mshikamano wa kitaifa.

Nawasalim kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-Acha kazi iendelee!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %