George Michael Uledi
Kyela,Mbeya.
April 30,2021.
Mama mmoja,msomi mtulivu na mbobezi wa siasa za Tanzania kuanzia ubunge, uwaziri,makamu wa Rais na baadae Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo anakwenda kuandika historia ya kipekee barani Afrika na labda duniani kwa ujumla!
Ni wazi kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan uwenda akapitishwa kwa kura zote za mkutano mkuu wa CCM kutokana na uwezo mkubwa wa uongozi aliuonyesha ndani ya muda mfupi ndani ya Serikali tangia kuapishwa kwake mwezi Jana!
Hotuba yake wakati anahutubia Bunge ulitosha kumtambulisha wazi kwa wana CCM kwamba huyu ni mwenzetu na lazima twende nae pamoja kwani aliweza kuhakikisha kuwa utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020 mpaka mwaka 2025 inatekelezwa kwa kasi kubwa.
Kwa sababu hiyo sitoshangaa kuona mama Samia leo anakwenda kuokota kura zotee ndani ya CCM na kuweka historia kubwa katika maisha yake binafsi,maisha ya CCM na maisha ya Tanzania.