0 0
Read Time:1 Minute, 30 Second

Na Dr Yahya Msangi

TOGO West Africa.

Dr Yahya Msangi

Tumezoea kusikia wageni Afrika Kusini wakishambuliwa na wenyeji. Tatizo hili la XENOPHOBIA limejikita nchi nyingi za Afrika, Ulaya na Marekani. Ukiwa Marekani au Ulaya mtu akijua wewe wakuja tusi la “go back home” litakuhusu. Hakika ni Tanzania pekee imeweza kuzika xénophobie ! Falsafa ya TANU ya “BINADAMU WOTE NI NDUGU ZANGU NA AFRIKA NI MOJA” imefanya kazi sawasawa. Hakika hakuna kama JULIUS KAMBARAGE!Kwa West AFRIKA xenophobia ipo sana! Mifuko ya viroba jina maarufu ni GHANA MUST GO HOME! Ukifika sokoni ukisema “nipatie Ghana must go home” utaeleweka. Asili ni wanaijeria kuwataka waghana waliokimbilia Nigeria kipindi cha mapinduzi kadhaa ya kijeshi warudi kwao. Waghana wakafurushwa na viroba vyao wakaacha maduka na mali zao zikiporwa. Hapa Togo ukisikika unaongea kiingereza mara moja utasikia “mu Ibo au naijeria man or american huyo”! Kabila la Ibo halipendwi kuliko wahausa, fulani, yoruba n.k. Watogo wanaamini kwa dhati wa Ibo ni wezi na wana uchawi mkali. Eti wakitaka bibi wanatumia uchawi kumpata na wakitaka héla wanatoa kafara mtu. Lazima useme fasta mie Mtanzania la sivyo utaona ama wananuna ama wanaondoka! Kuna wakati ulizuka mgogoro wa kidiplomasia kutoka na magari ya wanaijeria kusumbuliwa mnoo na polisi wa trafiki.Lakini wiki iliyopita kumetokea mpya nchini Cote d’ Ivoire. Kulikuwa na mitandaoni picha ikionyesha kuwa nchini Nigeria kuna raia wa Cote de Ivoire wameshambuliwa na kuuawa. Mjini Abidjan kuna kitongoji cha wanaijeria kinaitwa LITTLE LAGOS. Basi watu wakaenda kukishambulia, kupora, kujeruhi, kubaka na inasemekana kuua wanaijeria! Eti wanalipiza! Baada ya tukio ikabainika kilichokuwa mitandaoni ni feki! Sasa kuna sintofahamu kati ya Nigeria na Cote D Ivoire. Serikali ya Nigeria inataka fidia na waliohusika wafikishwe mbele ya mkono wa sheria!Ukitizama haya hutasita kuitamani Tanzania! Kweli tazama ramani utaona nchi nzuriii, nchi yenye mabonde mengi ya nafaka!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %