Dr Yahya Msangi
TOGO WEST AFRICA 🌍
“Uranium tunayo, wataalamu tunao Nini kinatufanya tusitengeneze bomu la nyuklia? Nani kasema ni haki mipanya kuwa na nyuklia lakini ni haramu sisi kuwa na kakwetu ka kujilinda na kuzalisha nishati?”
Mwanzoni jamii na mataifa yalipigana ili kumiliki kizazi (DNA WARS). Ilikuwa fahari damu au vinasaba vyenu kuwa ndio vingi. Hâta ujerumani akajikita kwenye ARYAN BLOOD. Akitaka Aryan Blood itawale dunia.
Mataifa na jamii vikaachana na DNA WARS vikaanza SPIRITUAL WARS. Vita vya imani za kidini. Ndiyo yakaanza ma crusade. Kila mmoja akitamani imani yake itawale dunia. Hâta wa mizimu wakabatizwa na kusilimishwa kwa hiari au kwa nguvu.
Baadae jamii na mataifa zikajikita kwenye vita vya kiitikadi (IDEOLOGICAL WARS). Yaani Kila mmoja akitaka itikadi yake ndio itawale dunia. Capitalism, Socialism, Communism, Ujamaa, Duche, etc.
Sasa dunia iko ngazi nyingine. Sasa hawajali cha damu, dini ama itikadi. Sasa ni vita ya kugombea mali asili (NATURAL RESOURCE WARS). Hakuna mgogoro au vita hapa duniani siku hizi ambao chimbuko sio kugombea resources. Utapakaziwa ni DNA, IDEOLOGY, SPIRITUAL lakini ndani kabisa ni dhahabu, uranium, maji, tanzanite, cobalt, coltan, bauxite, etc.
Hâta Middle east utakuta mfano maji ya mto Jordan ndiyo kiini Cha ugomvi usioisha Kati ya Israel, Jordan na Syria. Maji ya Nile Eneo la Suez Canal ndiyo kiini cha ugomvi na vita baina ya Israel na Egypt. Haya hayawekwi hadharani maana kuna mmoja ataonekana dhahiri ni mwizi!
Sasa hivi Egypt na Ethiopia wako kwenye fukuto linaloweza kusababisha vita. Kisa maji! Kwa Afrika Mashariki kaeneo kenye mawe lakini kamezungukwa na samaki nusura kilete vita Kati ya Kenya na Uganda!
Sasa ukiwa na utajiri wa mali asili ujue utalengwa utake usitake. Utajibaraguza wee kuzuia lakini iko siku mipanya itatoboa ukuta!
Na mipanya ina hila, nguvu na uwezo wa kutoboa ukuta. Ukikinga kifua wanakipasua paaaaaa!
Wajanja ni wale ambao wako busy nao kutengeneza nguvu ili mipanya iwaogope. Na wamegundua ukimiliki nuklia mipanya haisogei! Cuba alijipima akaona siwezi kutengeneza nuklia. Akawaalika warusi waweke nuklia Havana. Hawagusiki japo wako jirani na panya mkuu!
China, Korea Kaskazini, Irani, Pakistan, India na Urusi wakaona isiwe tabu ngoja nasi tutengeneze nuklia! Hawagusiki! Mapanya yatanguruma weee lakini kutoboa ukuta yanasita! Assad, Gaddafi na Sadam walihadaiwa kuachana na kutengeneza nuklia! Mapanya yamejaa télé yanacheza rege vyumbani.
Nchi za kiafrika zinahadaiwa! Ooo nyuklia ni hatariii. Inachafua maziingiraa. Hamna akili mtaitumia vibayaaa! Na waafrika tumekubali. Tuna majeshi ya kubeba SMG! Yataweza mipanya ikija?
Uranium tunayo, wataalamu tunao Nini kinatufanya tusitengeneze bomu la nyuklia? Nani kasema ni haki mipanya kuwa na nyuklia lakini ni haramu sisi kuwa na kakwetu ka kujilinda na kuzalisha nishati?
Siku hizi ukijifanya hutaki kuuza madini walau upate hela utakuja kushangaa siku mipanya ikija na kuchukua buree! Tizameni mafuta ya Libya, Iraq na Syria! Mipanya inafyonza bureee!
Uza makenikia, uza tanzanite sasa!
Tafuta bei nzuri uza wekeza kwingine. Natamani musome kitabu cha mtawala wa Dubai Makhtoum Al Makhtoum ! Yee anauza mafuta sanaa anawekeza kwenye IT na Commerce. Mambo ya kuvundika mali ardhini ije kuibwa na mipanya hataki!
Tumeelewana?