0 0
Read Time:1 Minute, 3 Second

Na H.Mkali

UK.

Hapa nina hofu hawa watu (wanaojiita wa nchi zilizoendelea) wana azma ya kutuingiza kwenye madeni yasiyolipika “incrementally” kama walivyofanya miaka 1980s. Yaani kila “variant” ya corona itakayojitokeza watupe mkopo, huo upuuzi mwisho wake utakuwa wapi?

Matokeo ya kushindwa kulipa madeni ya nyuma ilikuwa ni (IMF & World Bank) kutuletea kitu kilichoitwa “Structural Adjustment Programmes (SAPs) zilizotulazimisha nchi za Dunia ya Tatu tufute sera zetu za kutoa elimu, huduma za afya bure, tufute ruzuku zote kwa wakulima wetu nk nk. Hizo SAPs tuliletewa ili tuweze kulipa madeni yao – madeni ambayo yalikuwa “pushed on us.”
Na huku kulikuwa ni kutunyang’anya uhuru kinyemela. Ndiyo sababu Mwalimu Nyerere aliwahi kuhoji wakati huo kuwa: “… tangu lini IMF kirefu chache ni International Ministry of Finance?”

Lakini wakati huo huo wanatuzuia sisi tusitowe misaada kwa wakulina wetu, kwa mfano, asilimia zaidi ya hamsini ya bajeti ya Umoja wa Ulaya ilikuwa wanapewa wakulima wao, tena bure siyo mkopo,

Hawa wanataka kuturudisha kwenye enzi za SAPs kwa mlango wa nyuma Tanzania tuwe macho sana. Msimamo wa Hayati Magufuli kwenye hii mikopo ya corona ulikuwa ni kuntu, ulikuwa hauna dosari kabisa.

Tusiwe “naive” chonde, chonde. World Bank na IMF hapa wanawakilisha maslahi ya ‘Big Pharma’ na siyo sisi, tusijidanganye.

mkali@live.co.uk.
07/06/2021.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %