Na Mwandishi wetu, Dar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Balozi za Tanzania kuainisha na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini hususani biashara na uwekezaji.
Dkt. Mpango ametoa maelekezo hayo alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam. Mara baada ya kuwasili katika banda la Wizara, Dkt. Mpango amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
“Naipongeza Wizara kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ……..lakini pia Wizara iendelee kuzishirikisha Balozi zetu katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini, na Balozi hizo ziainishe fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nchi za uwakilishi kwa ajili ya Watanzania,” Amesema Dkt. Mpango
Pamoja na mambo mengine, Dkr. Mpango ameielekeza Wizara ya Maambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kuboresha majukumu ya Wizara ikiwa ni pamoja na balozi za Tanzania na Taasisi zake.
Read Time:54 Second