0 0
Read Time:4 Minute, 11 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 13,2021.

Ukitaka kupima uchumi wa Taifa fulani au Nchi fulani ni uchumi wa kisasa au uchumi wa kizamani,angalia soko la bima katika uchumi husika!Uchumi ambayo hauambatani na kukua kwa sekta na masoko ya bima kwa hakika huo ni uchumi dhaifu na usioweza kuhimili labsha za hapa na pale za kiuchumi.

Ni wazi kujua kuwa, matishio ya kiuchumi ni ya kawaida katika dunia ya leo,matishio mengine yakiwa ni “predictable na mengine yakiwa “unpredictable” kwa hiyo, Uchumi wowote wenye maono makubwa, moja ya viashiria vyake ni ukubwa wa sekta ya bima katika uchumi husika!”Insurance covarage”

Jukumu moja wapo kubwa la viongozi wa kisiasa lilipaswa kujua mambo mengi ya msingi ambayo yanaweza kuathiri uchumi katika maeneo yao ya utawala!Kwangu mimi, Kiongozi anayejua wajibu wake kama RC,DC hata Waziri wangeweza kuzilazimisha baadhi ya biashara katika maeneo yao kuingia katika mfumo wa bima kwa lazima!

Natolea mfano,nani alijua kuwa vurugu na maandamano ya Afrika Kusini leo yangeweza kuleta madhara makubwa kwenye uchumi wa wafanyabiashara na watu binafsi!Nyumba zinachomwa moto,magari yanachomwa moto, maduka yanaibiwa,kwa kifupi biashara na uchumi mzima wa afrika Kusini leo unabomolewa na wafrika Kusini wenyewe!

Swali hapa je,ni nani ataweza kurudisha hasara hii kubwa katika uchumi wa Nchi husika baada ya kukoma kwa maandamano hayo?Je,ni Serikali au watu binafsi!?,Na hapo ndipo dhana nzima ya bima uingia!Bila bima au bila “stimulas package”, uchumi wa Afrika Kusini katika miji kadhaa unaenda kusinyaa!

KITU GANI VIONGOZI WA KISIASA LAZIMA WATUSAIDIE KATIKA MAENEO YAO YA UTAWALA?

1.Shirika la Bima la Taifa linapaswa sasa kustuka na kuanza kuwapa semina kuanzia na Mawaziri,Marc na Madc kuhusu nini maana ya bima katika kulinda chumi katika maeneo yao ya utawala!Mfano,thamani ya biashara katika Jiji la Dar es salama pekee yake ni karibia nusu ya uchumi wa Taifa hivyo janga lolote ambalo litaigusa Dar es salaam leo linaweza kusababisha mdororo mkubwa wa uchumi!

Mfano,hivi inakuwaje Kariakoo leo ikapigwa na magaidi?hivi inakuwaje leo Mwanjelwa Mbeya ikapigwa na magaidi?,hivi inakuwaje leo Makoroboi Mwanza ikapigwa na magaidi?,hivi inakuwaje Wilaya kama ya Chunya ikapigwa magaidi?!Katika maeneo yote niliyotaja hivi inakuwaje janga kubwa la moto laweza kuwa la kutengenezwa”sabotage” au ajali ya kawaida likatokea!

  1. Case study za majanga ya moto katika maeneo ya Kariakoo,NMB Kasulu na shule mbili za Sekondari za Mkoani Morogoro kuungua moto zingeweza kuwa ndio “baseline” ya kuanzisha kampeni kubwa ya kitaifa kwa Shirika la Bima la Taifa ili kuwashawishi wafanyabiashara katika kujiunga na bima ya majanga katika maeneo yao!

3.Moja la jukumu au kipimo cha Mkurugenzi wa Halmashauri,afisa biashara kingeweza kuwa ni kwa jinsi gani ameweza kushawishi biashara kubwa na kati kuingia katika bima ya Taifa!Kwa kufanya hivyo tunakuwa tunalinda Uchumi wa Taifa na biashara katika maeneo yetu kwani biashara ni ajira,biashara ni kodi na biashara ndio uhai wa banki zetu kwani biashara nyingi utegemea mikopo kutoka banki za biashara!

4.Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa “Tamisemi” lazima zichukue wazo ili na kulifanyia kazi haraka kwa ustawi wa uchumi mkubwa wa Taifa.Fikilia ni kiasi gani cha kodi Serikali itakosa pale sokoni Kariakoo?Ni wazi kuwa gharama ya bidhaa mitaani kwa maana ya Tabata,Keko,Kimara,Mbezi na kwingineko zinaenda kupanda kutokana na kuungua kwa soko hilo!

Gazeti la Citizen la July 13,2021 limeandika kuwa, mpaka jana hakuna mfanyabiashara hata mmoja kutoka sokoni Kariakoo ambaye ameshafungua madai ya bima kitu ambacho kinatoa tafsiri kuwa karibia biashara nyingi za kariakoo hazijakatiwa bima!Hii ni hatari katika kujenga uchumi wa kisasa!

5.Nilitegemea Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, alipotembelea soko la Kariakoo baada ya kuungua ajenda yake ya kwanza ingekuwa kuuliza kuhusu bima na kusisitiza umuhimu wa biashara kuwa na bima katika kila size!Hakukuwa na haja ya kuongea na Banki kuhusu kusogeza mbele makato ya mikopo kama biashara zile zingekuwa na bima!

USHAURI WANGU KWA KILA TAASISI NI HUU HAPA!

1.Kuna siku kama Taifa tunaweza kujikuta katika mkwamo mkubwa wa kiuchumi kwa sababu tu ya kushindwa kusimamia mambo ya msingi katika chumi zetu na gharama yake ikawa kubwa!Nashauri suala la bima katika biashara liwe la lazima na viongozi wa kisiasa waanze kusimamia ili katika maeneo yao!

2.Shirika la Bima la Taifa lazima liwe na vision kubwa na kujua jinsi ya kufanya “lobbying” kwa wanasiasa ili kuongeza wigo wa biashara kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanalinda uchumi wa Taifa!

3.Vyombo vyetu nyeti vya ulinzi na usalama lazima pia vijue kuwa hii ni ajenda kubwa na inapaswa kupewa kipaumbele na vyombo husika!Jukumu la kulinda Uchumi wa Taifa kwa idara yetu ya Usalama wa Taifa ni lazima!Nashauri idara ingepush sana suala la bima katika chumi zetu na katika biashara kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya Taifa!

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Mhadhiri wa zamani,Vyuo Vikuu Saut & Tumaini,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %