0 0
Read Time:1 Minute, 47 Second

Na Dr Yahya Msangi

Togo -West Africa

Kuna masomo ubaoni Lakini hatutaki kuyasoma. Namheshimu sana Mzee Warioba. Lakini naye hasomi ubao. Na inashangaza maana mzee huyu aliwahi kuwa: waziri mkuu waziri wa katiba na Sheria, mwanasheria mkuu wa serikali na mwanasheria kamati ya kimataifa mkataba wa bahari. Huko kote hakuona umuhimu wa kurekebisha sheria! Anaona sasa jua linatua! Anyway ni mzee wetu.

Ben Ali, Mubarak, Netanyahu na Zuma, Netanyahu na Ben Ali ni somo tosha kwetu. Wote ni wahanga waliosababisha majanga kutokana na katiba kuruhusu washtakiwe.

Ben Ali alikubali kuondoka pale alipohakikishiwa kuwa hatashitakiwa akiondoka. Ni Qatar ndiyo ilitafuta huu muafaka. La sivyo Ben alikuwa tayari akomae mpaka kieleweke. Majeshi yakiluunga mkono. Ni dhahiri damu nyingi ingemwagika na labda asitoke.

Likaja sekeseke Misri. Wakafa wengi. Mubarak “akajiuzulu” na “akashitakiwa”. Akaingia Mursi. Akapinduliwa na kushtakiwa kama alivyokuwa akidai Mubarak ashitakiwe! Mubarak akafikishwa mahakamani tena kwa machela. Hatimaye akawa huru! Mursi akafa! Misri haikupata faida yoyote kwa kumshitaki Mubarak. Iliambulia hasara tena upande wa upinzani ndio zaidi.

Ikafika zamu ya Netanyahu! Wanamuita “The Butcher of Tel Aviv”. Ikawa kila siku uchaguzi. Hataki kuondoka maana walishamfikisha mahakamani. Kinga ni uwaziri mkuu. Naye akaapa sitokiii! Akiona uchaguzi umekaribia anafanya kila hila itokee vita na wapalestina! Wanakufa wapalestina na waizraeli kisa abaki madarakani. Akaendelea wee mpaka siku akafanyiwa ‘uyuda’ na rafiki yake! Sasa yuko mahakamani na mwelekeo atafungwa. Chama châke hakikubali. Kimeanzisha harakati za kuwafarakanisha waizraeli wenyewe kwa wenyewe! Ili ionekane Netanyahu ndie anamudu nchi uchaguzi uitishwe arudi!

Sasa zamu ya mzulu Jakobo! Nchi imeingia balaa. Uporaji, uchomaji na mauaji! Kisa kafungwa!

Ni hivi: kuruhusu raisi au mkuu wa nchi kushitakiwa sio jambo la busara. Hâta huko kwa wakubwa ni nadra kusikia raisi mstaafu kafungwa! Hebu nitajie tuone wako wangapi? Au unadhani wao sio majizi? Marekani kinawasumbua hicho licha ya kuwa na katiba ya miaka 200! Mkuu alipohisi kifungo kinakuja akahamasisha wahuni wavamie bunge na kunya ofisi ya Spika! Yaani muingie ofisi ya Job mshushe magogo kama njia ya kutaka raisi abaki madarakani!

Kipengele hiki kwenye katiba yetu kibaki hivyohivyo. Kwanza marais wetu sio wezi wa kutisha na tunajua sanasaana miaka10 anasepa.

Si ndio banyanda na bagikulu? Naheene lolooo! Wabeja koloomba!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %