0 0
Read Time:5 Minute, 0 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 15,2021.

Ilikuwa usiku wa kifo kwangu na wenzangu zaidi ya mia mbili, kamwe sitosahau na mara zote hii huwa ni “life unforgettable death experience”, baada ya kuanza safari ya masaa kumi na mbili usiku wa saa kumi kamili katika milima,mabonde na tambalale kuutafuta usiku wa kifo kuelekea zoezi la kutisha la “heavy heart” kwa kiswahili linaitwa “moyo mgumu”!Masikini ya Mungu, hakuna kati yetu aliyekuwa anajua nini kinaenda kutokea katika usiku ule wa kifo!

Upendo wetu baina yetu huwa wa milele kwa sababu ya kuunganishwa na jasho na damu zetu zilizovuja katika matukio kama haya kwa ajili ya Tanzania yetu!Umoja wetu ndio nguvu yetu na Tanzania yetu ndio roho yetu!Naweza nisieleweke sana katika hili lakini baadhi yenu mtakuwa mmelewa slogani hii!

Japo kulikuwa na maandalizi ya wiki mbili kuelekea zoezi hilo la hatari huku Wakufunzi wakicheka kinafiki kwa kutuonea huruma, maana walikuwa wanajua nini tunaenda kukutana nacho polini,ni usiku ambao kamwe hausahauliki mpaka kifo chako!Kwa kifupi naweza kusema nimewahi kuonja kifo kwa ajili ya kuilinda Nchi yangu Tanzania!

Yapata usiku wa saa tatu, tulianza zoezi kwa jacho na damu,kwa stiki na mateke,kwa matusi na mwishowe kubembelezana sababu wakufunzi wetu walikuwa wameshatufanya kila kitu wanachoweza ili kutekeleza zoezi lile lakini pale ndio ulikuwa mwisho wa akili zetu,nguvu zetu,Mungu wetu na dhamira yetu,haikuwezekana Tena!Yote hi vijana wale waliifanya kwa ajili ya kuilinda Tanzania yao hakuna kingine!

Huku kukiwa na karibia kilometa kumi za kutekeleza zoezi lile”heavy heart”,vilio vya maofisa vilianza mapema mno kiasi kwamba tulilazimishe wenyewe stiki,mateke na matusi toka kwa Wakufunzi zianze mapema!Tukiwa kilometa ya kwanza tu kati ya kilometa kumi,nadhani unaweza kupata picha ya usiku ule!Ndani ya kilometa moja tu ya zoezi lile mwili ulikuwa umegoma, japo roho ipo radhii!Hatari!

Yesu Kristo mwana wa Mungu,baada ya kuubeba msalaba ule kwa stiki na makofi nae aliwahi kusema”…..Roho ipo radhi lakini mwili huu dhaifu….” Baada ya kipondo cha kutisha kutoka kwa Askari wa Pilato!Na sisi ilifika kipindi dhamira ya kulifanya zoezi lile ilikuwepo lakini miili ya maofisa wale ilikuwa tayari ni dhaifu sana lakini pamoja na hali hiyo,Mzee wangu “King George” Mkingijage hakutaka kutuacha zaidi alisemaa”….maafaande hiyo ngoma lazima ifike hata kama ni asubuhi lazima ifike!Kweli ile ilikuwa kali na hakuna ofisa anayeweza kusahau katika maisha yake yote,ile kumbukumbu ni mpaka kaburini!

Kwanini niliamua kuanza na hii story?Nilitaka kuweka mazingira ya kuwaonyesha vijana wa kitanzania ambao mpaka leo wanaendeleza mijadala isiyo na tija kwenye social media dhidi ya Taifa kuhusu tozo katika miamala ya simu na tozo ya mafuta kwa ajili ya Tarura!Nikawa NAJIULIZA hivi,kama kuna vijana wanayatoa maisha yao kwa ajili ya Tanzania Je, kodi ni kitu gani?,kuna kilicho bora zaidi ya maisha?,kuna kilicho bora zaidi ya uhai?Hakuna!

UNAPOONA UBAHILI KULIPA KODI KWA AJILI YA TANZANIA FIKILIA PIA WALE WENZAKO WANAOYATOA MAISHA YAO KWA AJILI YA TANZANIA!

Gazeti la Mwananchi la July 15,2021 linaandika kwamba Tozo za Miamala ya Simu Kuanza Kung’ata Leo!Kwa maoni yangu wala sidhani kwamba tozo hizo zinang’ata Watanzania!Kwa kifupi gazeti ili limenisukuma kuandika ushuhuda huu kwa Watanzania wajue kwamba kuna watu “wanang’atwa” kwelikweli kila siku kwa ajili ya Tanzania lakini hawajawahi kusita kujitoa kwa ajili ya Tanzania na Taifa lao!

1.Tarehe isiyo na jina wala mwaka,kijana mmoja wa kitanzania ambaye alikuwa amemwacha Mama na Baba yake nyumbani na kwenda nje ya mipaka yetu kulinda maslahi ya Tanzania, hakuweza kurudi tena nyumbani baada ya majeshi ya Nchi fulani kumshuku kwamba anafanya shughuli zisizo za kawaida!Wakati akiwa katika harakati za kuokoa roho yake kwa kuvuka mpaka wetu na Nchi fulani kuwakimbia maadui, aliweza “kula” risasi zisizo na hesabu na maisha yake yakaishia hapo kwa ajili ya Taifa lake Tanzania.So sad!

Eti wewe leo, Tanzania anakuomba umchangie na umpe kidogo ulichonacho mfukoni kwa ajili ya barabara zetu za vijijini,unapiga kelele ambako huko kijijini ni mimi na wewe ndio tunakotoka!Aibu!

2.Mwaka usio na jina, katika Nchi ya Congo, waasi wa M20 wakati huo, waliweza kuchukua roho ya kijana wetu wa kitanzania mwenye cheo cha Ofisa akiwa katika uwanja wa medani!Ni habari ya kisikitisha sana!Ni kama sinema!Lakini Ukweli ndio huo!Nini tozo za Miamala bwana kuliko uhai!Biblia inasema..”mmepata bule toeni bule….”.

Inasemekana kijana huyo wakati yupo katika uwanja wa medani huko Congo, huku nyumbani mipango ya harusi yake ilikuwa inaendelea lakini harusi hiyo haikuwezekana tena baada ya waasi wale kukatisha uhai wake kwa ajili ya Tanzania!
Leo wewe Tanzania inakuomba kodi kidogo tu unapiga kelele!Aibu!

3.Mwaka na siku isiyo na jina “mdogo wangu” na member wangu wa zamani, Ofisa wa Jeshi “Komando”,alifariki dunia wakati akiwa kwenye zoezi la kujiandaa na siku ya Uhuru pale Dodoma!Vijana hawa sio kwamba hawajui wanafanya kazi ya kifo lakini kamwe hawajawahi kuhoji wala kupiga kelele na yote hii ni kwa ajili ya mapenzi yao mema kwa Tanzania!Wewe Leo unaombwa visenti kadhaa na Taifa lako Tanzania, unapiga kelele!Aibu kwenu!

Hakuna chenye dhamani duniani na kwa binadamu kama uhai wake, kwahiyo wale wote wanaopiga kelele kuhusu tozo mpya, nilitaka wayajue haya labda walikuwa hawajui!Wenzenu wanatoa uhai kwa ajili ya Tanzania ninyi mnapiga kelele kwa ajili ya vipande vya fedha!Aibu kwenu!

Tunapaswa kuipenda Tanzania kama ambavyo tunavyowapenda Mama zetu,wake zetu,waume zetu,watoto wetu na lazima tukumbuke kuwa bila Tanzania hata hicho kipato tusingekipata kwahiyo hata hiyo miamala tusingeifanya kamwe!

Kuna sehemu katika bara la Afrika hili hawazungumzii miamala na makato ya kodi tena bali wanaangaika na kuzungumzia jinsi gani watairudisha na kuipata amani katika Nchi zao lakini kwako wewe ni tofauti, Tanzania kukupa amani kwa zaidi ya miaka sitini je,wewe unampa nini Tanzania?

Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu wa Rais wa zamani,Daruso- IJMC,Mhadhiri wa zamani,VYuo Vikuu Saut na Tumaini,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari- Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,TMA Monduli Arusha,Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %