0 0
Read Time:1 Minute, 39 Second

Umetoa 113,000.00 Tsh. Kwa wakala: HENRY MWASHIGALA.Makato Tsh 6,130.00( Ada Tsh 3,600.00 + Kodi Tsh 2,530.00).Salio Jipya Tsh 870.00. Muamala No: CO210716.1408.B05841

Ni vizuri binadamu tukaishi kwa mifano kwa ajili ya kuwafanya wengine waamini kuwa kumbe “it can be done”.Leo niliona nianze na zoezi moja kwa ajili ya Tanzania yangu!

Kaka yangu na rafiki yangu mmoja kutoka Nchini Italy aliniletea kamzigo”fedha”kidogo kwa ajili ya weekend hii kama Shilingi 120,000 Tsh,asante sana kaka yangu kwa upendo wako mkubwa kwangu!

Baada ya kupokea “cash” hiyo soon niliamua kwenda kwa wakala wa Airtel money kwa jina hapo juu kuweka fedha hiyo!Lengo langu kubwa ilikuwa kuweka fedha hiyo kwenye Airtel money account na baadae jioni niweze kutoa fedha hiyo ili Serikali ya Mama yangu na Rais wangu Samia Suluhu Hassan iweze kupata haki yake.

Katika 120,000 Tsh ya niliyoweka kwa account yangu ya simu,baada ya kutoa fedha hiyo, nikajikuta nimekatwa kiasi cha Tsh 6,130.00 tu!Hakuna kitu kizuri kwangu kama kuchangia maendeleo ya Tanzania yangu!Najipongeza kwa hilo.

Hakuna kitu kikubwa ambacho mtanzania unaweza kujivunia kama kuchangia maendeleo ya Nchi yako kupitia kodi!Wenzetu ulaya wanapenda kuchangia maendeleo yao kwa kulipa kodi.

Lipa kodi ili uweze kumdai vizuri Rais wetu na Serikali yake kuhusu maendeleo yako!Hii ndio give and take ambayo matokeo yake tunaweza tusiyaone leo lakini naamini baada ya mwaka huu wa fedha tunaweza tukajustify rationale ya kuwepo kwa makato haya!

Lipa kodi ili tuweze kuibana vizuri Serikali yetu!Kulalamika kwa sasa hakutatusaidia sana!Twendeni tukaweke fedha zetu kwa simu zetu ili kuchangia na kusukuma maendeleo yetu kwa haraka zaidi.

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani wa Daruso-IJMC,Mhadhiri Msaidizi wa zamani vyuo vikuu vya Saut na Tumaini,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari- Maelezo,Ofisa mwanafunzi wa zamani,Chuo cha maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela mwaka 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %