George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 21,2021.
Mwendelezo huu wa kauli tata za makada wa CCM kwa sasa, ambazo hapo kabla tulikuwa tunaziona zinatolewa na CDM je,ni ishara kwamba Wanachama wa ccm kwa sasa hawatishwi na Chama chao tena au ni ishara ya kuendelea kukomaa kwa demokrasia ndani ya Chama chetu.?yote mawili yanawezekana!
Miaka mitano nyuma CCM kitaasisi ilionekana kuheshimika dhidi ya wanachama wake ndani ya Chama na ndani ya Serikali yenyewe,isingetarajia kuona kauli za namna hii kutoka kwa kada wa ccm au kutoka kwa ofisa wa Serikali kwenda kwa Watanzania!Chama kilishika hatamu kwelikweli,I stand to be corrected nikiwa sipo sawa!
Uzoefu wa miaka kumi nyuma unaonyesha kuwa uimara au udhaifu wa ccm mara zote umetokana na “either” kupuuza maslahi ya watanzania wanyonge au kuambatana na maslahi ya Watanzania wanyonge!Mafanikio au anguko letu uanzia katika mambo hayo makuu mawili,labda kama sijui vizuri!mifano hii hapa!
1.Waziri wa fedha wa wakati huo,Baziri Pesambili Mramba aliwahi kutoa kauli ya dhihaka dhidi ya Watanzania na matokeo yake yalikuwa kuongeza chuki ya wananchi dhidi ya Serikali yao!Wakati huo Serikali ilikuja na hoja ya kununua ndege ya Rais kwa ajili ya safari na Watanzania wengi walipinga sana!
Baziri Mramba aliwahi kusema”….hata kama Watanzania watakula majani lakini ndege ya Rais lazima inunuliwee…”.Kauli hiyo iliwafanya Watanzania wengi kuamini kuwa Serikali ya ccm ilikuwa imejaa jeuri na dhihaka kwao na matokeo yake ilikuwa ni kuenea kwa upinzani kila kona ya Tanzania!
Kwa kifupi,matendo ya hovyo yaa wanaccm ndio yalizalisha upinzania na sio kwamba upinzani ulikuwa na hoja na mipango ya maana ya maendeleo kwa Watanzania!
2.Juzi juzi kuelekea Uchaguzi Mkuu ndani ya ccm katika Jimbo la Uchaguzi Kyela,Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo ndugu Harison Mwakyembe katika hali isiyotarajiwa na Watanzania wengi aliweza kukataliwa kwa kura za mkutano Mkuu wa ccm wa Wilaya ya kyela na kushika nafasi ya tatu!
Kauli zake za majigambo dhidi ya wananchi na wanaccm zilifanya Wilaya nzima ya Kyela kuanza kumshambulia hasa pale aliponukuliwa akisema”….mnalia maji ya kunywa wakati mungu kawapa mto kiwira….”.lakini kauli yake ya pili kwamba yeye hakuja kugombea sababu ya njaa kwani tayari alikuwa na kazi yake nzuri hapo kabla nayo iliwafanya wana Kyela kufikilia mara mbili mbili kumpa kura!
Kauli mbaya zaidi ni ile ya kusema “ndio tatizo la nyie darasa la saba” ambayo ilitafsiriwa na wajumbe wa mkutano ule wa CCM Wilaya kama dharau kubwa kwao!
Kwa kauli zile,wanakyela walishaapa kuwa endapo atapitishwa na ccm kugombea Jimbo Lile basi Walikuwa tayari kumpigia kura Mgombea wa CDM Ndugu Alinanuswe Mwalyange!CCM ikastuka na haikurudisha jina la Ndugu Mwakyembe!Na hii ndio ilikuwa pona yetu pale Kyela!
3.Kauli ya juzi ya Waziri wa fedha, Ndugu yangu mwigulu Nchemba, imezua mjadala na hasira za wananchi dhidi yake mwwnyewe na dhidi ya Serikali ya CCM.Katikati ya vuguvugu hili la tozo ya miamala ya simu Mwigulu hakupaswa kabisa kutoa kauli ya kuudhi kama hii!
Sio tu kwamba kauli ile imewaudhi Watanzania lakini pia kauli ile inaweza kabisa kuharibu mahusiano ya kidiplomasia kati ya Burundi na Tanzania na jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.”EAC”.
Kauli yake ni wazi inaifanya Serikali ya awamu ya sita kuonekana kwamba “inapandisha mabega” kwa wananchi kitu ambacho Mh Rais Samia Hassan alishatoa tahadhali mapema kabisa!Je,Mwigulu hakusikia?
Rais Samia Hassan anajua gharama za kupandisha mabega kwa wateule wake dhidi ya wananchi ikoje,Rais anajua lakini wateule wake wanaonekana kutokujua hilo!
NAOMBA KUSEMA LOLOTE NA CHAMA CHANGU NA SERIKALI YAKE YA CCM.
1.Mwigulu Nchemba alipaswa atupishe kwanza katika nafasi yake kwa sasa kama ishara ya mamlaka ya Uteuzi kuomba radhi kwa Warundi na Watanzania.Hii inaweza kutuokoa na hasira za wananchi dhidi ya tozo za miamala ya simu lakini pia dhidi ya kauli yake ya dhihaka!