
Wabongo ughaibuni Wu
Na K@2021
Nimegundua kuwa Watanzania wengi wanapenda nchi yao Sana na wanatamani kuona Nchi inapata maendeleo na Maisha ya Watanzania yanakuwa mazuri. Watanzania wanapenda kuona nchi yao iko salama na kuimarika kwa Amani, nimegundua kuwa Watanzania waliupenda Sana uongozi, falsafa,uthubutu na uchapakazi wa Hayati Dr John Pombe Magufuli. Kuendelea kusononeka na kulia haita tusaidia kitu, tukumbuke watu wa aina ya Dr John huja kwa makusudi ya Mungu na kawaida hawakai Sana,mara wanapomaliza mission yao huondoka.
Dr Magufuli ametuachi elimu kubwa yenye muongozo na dira ya nchi yetu sasa na vizazi vijavyo,ndio maana wasia wake karibu na mwisho alisema kuwa ” Ndugu zangu ipo siku mtanikumbuka na najua mtanikumbuka kwa mema kwa kuwa nime sacrifice maisha yangu kwa ajili yenu “
Dr Magufuli alimaanisha kuwa ikiwa tutafuata falsafa yake ni dhahiri tutafanikiwa kama nchi na tutafika kule alipodhamiria kutupeleka hivyo tutamkumbuka kwa mafanikio, na vivyo hivyo ikiwa kinyume chake tutamkumbuka kwa kujuta kudharau aliyotuachia kama muongozo.
Nimegundua Watanzania wengi wamepata kujitambua katika kipindi Cha uongozi wa Dr Magufuli ,amefanya watu kutambua kuwa wanaweza,Sio masikini kama walivyo aminishwa na mabeberu, Watanzania wameweza kutambua uhuru wa kweli ni kumiliki rasilimali zao ambazo ndio nguvu ya Uchumi wa nchi. Watanzania wametambua kuwa na nguvu kubwa ya Uchumi ndio njia pekee ya kulinda uhuru wao wa kweli bila kutegemea mataifa ya magharibi. Falsafa ya Dr John Pombe Magufuli imewafunza Watanzania kuwa wajibu wa viongozi wa umma ni kutumikia jamii na Sio ubwana, vivyo hivyo imewafunza Watanzania kama raia Wana wajibu Mkubwa kuchapakazi kwa bidii na kuchangia maendeleo ya nchi Pamoja na kuhakikisha amani ya nchi inadumu.Falsafa ya Dr John Pombe Magufuli ni pana Sana kuichambua na kuielezea, lakini itoshe kusema Hayati ameacha amekwisha panda MBEGU ya uzalendo wa kweli.
Ushauri wangu,ili tuendelee kumuenzi mpendwa wetu na shujaa wa Taifa letu,ni lazima kuungana na mrithi wake ambae ndie mwenzi wake tangu alipoingia katika mchakato wa kunadi ilani ya Chama na kuomba ridhaa kwetu, kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza falsafa ya umoja na mshikamano jambo ambalo Hayati kipindi chote Cha uhai wake amekuwa akihubiri Amani, upendo na mshikamano huku akisisitiza .. *
“Ndugu zangu tusibaguane,kwa kabila zetu,dini zetu au itikadi zetu za kisiasa” Tuna wajibu wa kumuunga mkono Mh Rais wetu SAMIA SULUHU HASSAN kwani kwa kufanya hivyo tutamtia nguvu hata ya kufanya maamuzi katika kusimamia maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu.
Mh Rais ametupa uhuru wa kuikosoa Serikali na kuishauri,ila lazima tutumie lugha za staha kama ilivyo tamaduni zetu Watanzania.
Mimi binafsi kifo Cha Hayati Magufuli kilinipa mshituko Mkubwa kiasi ilinichukua muda mrefu kuamini kuwa shujaa wetu ameondoka, mtu ambaye alifanya hata Watanzania wanaoishi nje kutembea kifua mbele na kujisikia fahari kujitambulisha Uraia wao wa asili. Naamini mamilioni ya Watanzania ndani na nje kila mmoja aliathirika na msiba wa shujaa wetu kwa namna yake,na uthibitisho ni mazishi yake yaliacha dunia nzima ikistaajabu.
Ni wakati sasa bila kusahau tulipotoka kama Taifa,kuungana na Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuchapakazi kwa bidii, kuisemea na kuitetea Serikali na Rais wetu,huku tukiitanguliza Nchi kwanza, huu ni wakati wa kuidhihirishia Dunia kuwa Tanzania iko imara hata katika mtikisiko Mkubwa Bado tuko Pamoja. Tukosoane bila kutoa mwanya kwa maadui wa Taifa letu ambao wanaweza kupenyeza ajenda zao za Siri ili kutuvuruga na kuweka Amani ya nchi yetu kuwa mashakani. Katika kipindi Cha awamu ya tano tumeona watu hasa wanasiasa walio jipambanua dhahiri kuwa ni vibaraka wa mabeberu,wapo waliozunguka dunia nzima wakijipa Kazi ya kuchafua nchi yetu na serikali kwa ujumla huku baadhi wakipata kuungwa mkono na hata Watanzania wenzetu ughaibuni ili mradi watimize azma zao chafu kwa taifa letu. Wapo walioandika makala nyingi kwenye Media za nje lakini wote hao walijibiwa na Watanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo Rais wetu SAMIA SULUHU HASSAN alizunguka nchi nzima akimsaidia Hayati Dr Magufuli kunadi Sera na ilani ya CCM huku wakiomba ridhaa ya Watanzania kuendelea kuwatumikia.

Mh Samia Suluhu Hassan

ANGALIZO:
Matatizo yetu ya ndani kamwe tusikubali kuyatoa nje kwa kutegemea tutapata majawabu kutoka mataifa ya magharibi au mengine ya Africa,tunao uwezo wa kumaliza changamoto zetu wenyewe.
Tusikubali kucheza Ngoma ya wachawi wa Taifa letu tukadhani ni watabibu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
KAZI IENDELEE NA #SSH