0 0
Read Time:4 Minute, 14 Second

George Michael Uledi
Kyela,Mbeya.
July 24,2021.

Bunge la Spika Job Ndugai la mwaka 2020 mpaka 2025, moja ya kitu ambacho lilipaswa kukitafuta ni “political ligitimacy”& kubeba sura kuu mbili yaani ya upinzani na pia sura ya chama tawala!Sababu kubwa ya kubeba majukumu haya mawili ya kuwa “opposition” na kuwa Chama tawala ni kubwa mbili;

1.Kutengeneza uhalali kwa wapiga kura”wanyonge” ambao waliamini kuwa CCM ya awamu ya tano pekee yake bungeni, ingeweza kuzibeba changamoto zao na kuzitatua kwa haraka kama ilovyokuwa ndani ya miaka mitano kuanzia 2015 mpaka 2020 ya utawala wa JPM!

2.Kuzima kelele za wapinzani ambao walizunguka mitandaoni kupiga porojo kwamba bunge la asilimia 90+ ya Wabunge wa CCM halitakuwa na ufanisi kwa wananchi!Kwahiyo Bunge la Ndugai la 2020 mpaka 2025 lilipaswa kuwaprove wrong wale wote waliolibeza kabla ya kuanza kazi zake”one man show”.

Bunge la Ndugai lilipaswa kujua kuwa linabeba sura mbili hizo”dual role of a parliament”!Bahati mbaya sana mpaka dakika hii,sio Spika wao wala wabunge wenyewe wanajua hilo kuwa walikuwa wanabeba majukumu hayo makuu mawili”self regulation & control”.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %