0 0
Read Time:9 Minute, 29 Second

Makala hii imeandikwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Julai 24, 2021.

Baada ya kugonga mwamba kwa mpango chama cha CHADEMA wa kuanzisha vurugu kupitia kongamano la Katiba Mpya lililopangwa kufanyika Jijini Mwanza Julai 21, 2021, chama hicho cha upinzani kimemwaga mpango wake mzima wa kuanzisha vurugu Tanzania.

Taarifa za ndani za kikao cha Kamati Kuu cha CHADEMA kilichoongozwa na Tundu Lissu aliyeshiriki kwa njia ya mtandao kutoka Ughaibuni na Katibu Mkuu John Mnyika zimeeleza kuwa mpango wa kuzusha vurugu kwa lengo la kuivuruga Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan uliandaliwa tangu siku nyingi kwa mahesabu kuwa ungewasilishwa kwenye Kongamano hilo na kuwakabidhi vijana wa CHADEMA kuutekeleza.

Taarifa za uhakika zinasema CHADEMA ambayo imekataa kuchukua fedha za ruzuku kutoka Serikalini imepatiwa mabilioni ya fedha kutoka nchi za Ulaya aliko Tundu Lissu kwa lengo la kufanikisha mpango wa Kuivuruga Tanzania ili Serikali ya CCM iondolewe madarakani na fedha hizo zimepangwa kugawiwa kwa vijana watakaojitolea kupambana na vyombo vya dola. Fedha hizo zimeingia nchi ni na zingine zinaendelea kuletwa kupitia Balozi, Mashirika yasiyo ya kiserikali na nchi jirani.

Mpango wa vurugu umetangazwa na Tundu Lissu ikiwa ni maamuzi rasmi ya kamati kuu ya CHADEMA. Tundu Lissu ametangaza mpango huo huku akiubatiza kuwa “HATUA ZITAKAZOCHUKULIWA KUFUATIA KUKAMATWA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE ANAYEKABILIWA NA TUHUMA ZA UGHAIDI NA NJAMA ZA KUDHULU VIONGOZI WA SERIKALI”

Kupitia mpango huo CHADEMA imepanga kuunda kamati ya kimataifa ambayo itaongozwa na Tundu Lissu kupita duniani kote kwa nchi marafiki wa Tanzania wakiwemo wadau wa maendeleo kuwaeleza kuwa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ni hivyo zaidi ya uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli.

Kwamba kamati hiyo itakwenda duniani kuitangazia dunia kuwa Rais Samia ana mpango wa kuwatesa wapinzani na kuwabambia kesi nyingi za jinai kuliko hayati Magufuli.

Kwamba kamati hiyo itakwenda kuiambia dunia kuwa Rais Samia amepanga kuongeza wafungwa wa kisiasa kwa kuongeza viongozi wa vyama vya upinzani kuliko ilivyokuwa kwa Hayati Magufuli.

Kwamba wanakwenda kuiambia dunia isitishe uhusiano wa kiuchumi na kidiplomasia na Tanzania mpaka hapo itakapotekeleza matakwa ya CHADEMA wanaodai kuruhusiwa kufanya maandamano na kudai katiba mpya.

Kwamba kamati hiyo inakwenda kuziomba nchi marafiki zote duniani kusitisha misaada yote kwa Tanzania. Na itazungumza na wananchi wa nchi hizo na kampuni za uwekezaji kwamba wasiwekeze Tanzania kwa sababu ni hatari sawa na ilivyokuwa wakati wa Hayati Magufuli.

Kwamba kamati hiyo itaendesha kampeni ya kudai Katiba Mpya kinyume na maelekezo ya Rais Samia na itafanya makongamano ya kudai Katiba Mpya nchi nzima.

Tafsiri ya haya yote ni kuwa sasa ni rasmi CHADEMA imeamua kutafuta madaraka kwa nguvu, inataka kuchochea vurugu Tanzania ili kushinikiza mazingira ya kukamata dola, inataka Tanzania iwekewe vikwazo vya kiuchumi na Dunia na inavialika vyombo vya habari vya kimataifa kuichafua Tanzania.

Hapa ndipo Watanzania tuwe macho, tusikubali kuharibu nchi yetu, tusikubali kuvuruga uchumi wetu, tuwakatae vibaraka hawa wa mabeberu ambao wanatumika kutuangamiza na tusimame na Rais Samia Suluhu Hassan.

Tanzania ni nchi huru, ni nchi inayojiamulia mambo yake yenyewe. Mbowe na wenzake akina Tundu Lissu wasiruhusiwe kuiyumbisha nchi hii.

Narudia Watanzania tuwe macho sana. Kwa miaka kadhaa tumekuwa nchi yenye utulivu, hawa jamaa wanataka kuturudisha kwenye nchi inayopambwa na mapambano ya vyombo vya dola na raia, milipuko ya mabomu na risasi, watu kupata ulemavu na kumwaga damu na kuharibu taswira ya nchi yetu.

Hawa jamaa wanataka tupoteze mwelekeo mzuri wa maendeleo tunaokwenda nao, wanataka tuache kujenga miradi yetu mikubwa ya reli, barabara, madaraja, hospitali, shule, maji nakadhalika na badala yake wanataka tuwe tunashinda na kukesha tukibishana kuhusu dhamira yao ya kuchukua dola.

Hawa jamaa wanataka tuvurugane ili rasilimali zetu, madini, gesi, mafuta, ardhi, hifadhi za misitu na mapori vichukuliwe na wageni wanaowatuma na kuwafadhili ili hatimaye watuache Watanzania tukiwa vibarua, ombaomba na masikini wa kutupwa kama ilivyo Afrika Kusini.

Wanataka tupoteze uhuru wetu, tuwe nchi inayopangiwa cha kufanya na nchi nyingine, wanataka tuchekwe na wanataka tudhalilishwe ilimradi wao wapate madaraka.

Wanataka Watanzania turudi nyuma, tuwe masikini wa kutupwa, tukose huduma za kijamii kama matibabu, maji, chakula nakadhalika.

Wanataka Watanzania tupoteze ajira, tuharibu biashara zetu, tuue utalii wetu, tukose wawekezaji wa kuja kujenga viwanda na kulima mashamba makubwa.

Wanataka Tanzania irudi kuwa nchi ya kuombaomba, isiyokuwa na heshima duniani na wenye nguvu za kiuchumi waje watupande mabegani.

Narudia Watanzania tukatae. Naomba sana Serikali yangu isiruhusi upuuzi huu wa akina Mbowe na wenzake. Nchi yetu ina sheria na taratibu, zisimamiwe. Asionewe mtu lakini pia asitokee mtu akawa na uhuru wa kuvunja sheria na kuhatarisha usalama wa Watanzania na rasilimali zao kwa matakwa yake binafsi.

Mwisho nawaomba Watanzania wenzangu tuungane na Serikali yetu, tuungane na Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kujenga Tanzania nzuri kwetu. Rais Samia ni Mama mwenye dhamira nzuri sana na wanae. Tukifanya hivyo amini nawaambieni hawa jamaa watakwama.

Wasitutishe kuwa tutasusiwa na Jumuiya ya Kimataifa, hii ni hoja ya kipuuzi kabisa. Hakuna kitu chochote cha maana ambacho kinaweza kututisha kwa hoja hii. Jumuiya ya kimataifa ni muhimu lakini ni lazima tulinde maslahi ya Taifa letu machoni pa Jumuiya ya Kimataifa kinyume na hapo ni uzwazwa na tutachekwa kila mahali.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Makala hii imeandikwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Julai 24, 2021.

24 Julai, 2021

CHADEMA OFFICIALLY BEGINS TO DISTURB TANZANIA. LET US BE WATCHFUL.

After hitting rock bottom with CHADEMA’s plan to pass through the New Constitution conference scheduled for activities in Mwanza City on July 21, 2021, the party which approved the plan for its entire Tanzanian product plan.

An internal statement from the CHADEMA Central Committee chaired by Tundu Lissu who participated online from abroad and Secretary General John Mnyika followed a plan to incite violence aimed at disrupting the Sixth Phase Government of President Samia Suluhu Hassan. so much for the calculation that you would be presented at the Conference and hand over to the CHADEMA youth to fulfill.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %