

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 27,2021.
Unaweza kumlazimisha punda kwenda kunywa maji mtoni lakini unaweza usifanikiwe katika kumlazimisha kunywa maji hayo kwahiyo katika mazingira hayo mswaga punda anapaswa kutumia hekima na akili ya kujiaminisha kuwa punda wake hana kiu ya maji!Inabaki hivyo!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Suluhu Hassan ni kama alimua kutembea katika msemo huo baada ya kutangaza uhiari kwa Watanzania kuhusu kuamua kutumia chanjo ya uviko 19 au kutokutumia baada ya kuwasili Nchini wiki Jana!Hakuna busara kubwa kama aliyoichukua Rais wa Nchi,Samia Suluhu Hassan!
NINI KINATOKEA KWA SASA NCHINI TANZANIA?
1.Baada ya kuwasili kwa chanjo hiyo ya uviko -19 ni kama upepo unataka kubadilika ambapo baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa Serikali na taasisi zingine wameanza kuipigia debe chanjo hizo na kuwaamasisha Watanzania kutumia chanjo husika!
2.Hatua hiyo inamwinua askofu Gwajima na yeye kuanza kuhamasisha watu wasitumie chanjo hiyo kwa sababu ambazo yeye anasema ni za kiafya hivyo kutaka kuwaaminisha watu kuwa chanjo hizo zina madhara makubwa kwa afya ya baadae ya Watanzania.
3.Miongoni mwa makundi haya mawili kuna kundi halisemi ukweli kuhusu chanjo hizi hivyo kuwaweka Watanzania katika njia panda kuhusu kutumia au kutokutumia!Mimi ningekuwa Katibu Mwenezi Ndugu Shaka wala nisingetumia muda mwingi “kusilence” mjadala huu muhimu zaidi ningekuja na “scientific”hoja za kumjibu askofu Gwajima!Basi!
KWANINI HOJA ZA ASKOFU GWAJIMA ZINAONEKANA SIO NYEPESI HATA KAMA HAZINA UKWELI?
1.Miaka miwili sasa nyuma, Tanzania hii iliweza kuheshimika duniani kote kwa jinsi ilivyopambana na suala la uviko 19 hasa wimbi la kwanza ambalo linasemekana ndio lilikuwa na madhara makubwa zaidi kuliko wimbi la pili na wimbi la tatu!Hoja ya askofu ni kwamba kwanini tuchanje leo na sio Jana ambapo tishio la uviko 19 lilikuwa kubwa zaidi Nchini?
2.Wakati wa wimbi la kwanza na wimbi la pili,Serikali ya CCM iliweza kutuaminisha kuwa chanjo hizo hazipo salama sana kwa maisha yetu hivyo haikuwa wakati sahihi kwa Taifa kukimbilia kwenda kwenye chanjo ya uviko-19.Ni mwaka mmoja tu Serikali ya CCM imeamua kutuambia kwamba chanjo hizo ni salama!Kwanini katika mazingira kama haya askofu Gwajima hakose kuhoji?
3.Wakati Mh Rais anazindua chanjo hiyo kesho,bado hakuna taarifa za wazi kuhusu madhara na faida za kuchanja chanjo hiyo!Serikali kupitia kwa wataalam wake bado haijatoa taarifa “scientific prove” kuweza kuwaaminisha Watanzania kwamba usalama wa chanjo hizi upoje hasa wakati ambao Watanzania hawa walishaaminishwa na Serikali ya CCM ya awamu ya tano kuhusu madhara ya chanjo hizo.Je,Serikali imefanyaje kubadilisha hiyo hali?”altitude change”.
4.Anachotaka kuhoji askofu Gwajima ni je,tunataka kuachieve nini mpaka tukaamua kuipigia debe chanjo ya uviko na kwenda kuipokea Airport kwa mbwembwe nyingi?Je,tumewekewa malengo ya idadi ya watu kuchanjwa na watoa chanjo?if not,why tunatumia nguvu nyingi kutangaza au kuiponda?Kama suala ni hiari,kwanini tunatumia muda mwingi kuipamba na kuipigia kelele?
USHAURI KWA CHAMA CHANGU NA SERIKALI YANGU YA CCM.
1.Chanjo ya uviko 19 ni bomu kubwa kwenye siasa za ndani kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2025!Tuna mambo mawili ya kuchagua,tuendelee kusisitiza kuwa ni hiari au tuendelee kuipigia debe na maamuzi yote hayo yana faida na hasara zake kisiasa!
Watanzania wanahoji,kwanini tumeamua kuuza ushindi wetu na heshima yetu ambayo tuliipata kupitia mapambano dhidi ya uviko 19?,lakini pia Watanzania wanahoji,mbona gharama ya kuuza heshima yetu imekuwa “so cheap”?
- Serikali yangu ya CCM ikumbuke kuwa suala la uviko “it is so temporary”kwa maana ya chanjo,sidhani kama chanjo hizi zitakuwepo kwenye mjadala tena mwakani,lakini “political implications” yake inaweza ikawa ya muda mrefu kwetu na Chama chetu kuelekea 2025,twapaswa kuliangalia kwa umbali na upana wake suala la chanjo ya covid,kamwe Chama tusijiingize kwenye mjadala huo!
3.Ni wazi kuwa idadi ya Watanzania watakaopokea chanjo hizi itakuwa ndogo sana na sababu ni kuwa hakuna “altitude change intervations” za maana zilizofanyika toka Watanzania wavuke kwenye janga la kwanza la uviko 19 kwa kutumia njia za asili “nyungu”.
Katika mazingira hayo tusitegemee makubwa na hatua yoyote ya kutaka kuipush ajenda hii athari zake katika siasa za ndani zitakuwaje kubwa sana!Hatupaswi kupuuza hawa hata kidogo kwani sisi tunaoshinda kwenye social media tunaona yanayoendelea,tusikilizeni kwa maslahi mapana ya Serikali ya CCM .
Suala la chanjo ya uviko 19 Nchini tusipokuwa makini nalo pia linaweza kutugawa kama Taifa.Kauli ya Mh Rais kwamba chanjo ni hiari iheshimiwe kwani Rais labda alishasoma uwanja wa vita ukoje na nimpongeze kwa msimamo huo na ndio maana mpaka leo Mh Rais hajawahi kuipigia debe chanjo hiyo,debe lenu linatoka wapi?
Mwandishi ni Kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Serikali ya wanafunzi, Daruso-IJMC,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha na Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.








