0 0
Read Time:5 Minute, 2 Second

George Michae Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 28,2021.

Wakati Mh Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kupokea repoti siku chache zijazo kuhusu namna bora ya kutekeleza suala la tozo kwenye miamala ya simu, baada ya kuwepo kwa kelele nyingi mitaani, tayari Nchi nyingi za Afrika nazo ziliingia mkenge katika suala zima la uanzishaji wa tozo kwenye miamala ya simu miaka ya 2010.

Swali kubwa hapa ni je,wataalam wetu wa fedha na masuala ya kodi walishindwa kutumia uzoefu wa Nchi zingine za Afrika zilizotangulia kuanzisha tozo hizo ili kuweza kuja na mapendekezo mazuri zaidi ya kisera na kisheria katika suala husika?,kwanini wataalam wetu hawapo “aggressive” na kuonekana wamelala?!Kuna mifano kadha wa kadha barani Afrika, ambapo wananchi walipinga tozo hizi na kusababisha miswada/sheria za tozo hizo kusimamishwa hivyo kuharibu mipango ya kibajeti ya Serikali zao!

Tafiti zinaonyesha kuwepo kwa migomo ya tozo hizo Nchini Malawi,Kenya,Uganda,Congo,Ivory Coast na kwingineko na sababu kubwa ya kupingwa kwa tozo hizi zilikuwa pamoja na mambo mengine ni ukubwa wa tozo hizo pamoja na kuwepo kwa “double taxation” kwa mtu mmoja!kwahiyo ni wazi kuwa wataalam wetu walikuwa na “case study”nyingi za kutufanya kutorudia makosa ya wenzetu hivyo kuja na “version” bora ya “digital mobile money taxation”lkn hakuwezekana,hivi tunakwama wapi?

KWANINI WATALAAM WETU AFRIKA KILA MARA WANAZIINGIZA SERIKALI ZETU MKENGE?

1.Ni wazi kwa mfano, katika repoti tarajiwa ya “kitaalam” itakayokuja kwa Mh Rais, Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine, lazima itapendekeza baadhi ya mabadiliko ya kikanununi katika baadhi ya maeneo ambayo kwa vyovyote yatapelekea kushindwa kufikia malengo ya kibajeti ya Serikali yalikusudiwa hapo awali!Je,nani anabeba hasara hiyo?Nakumbuka wakati ule,hapa suala la kutumbuana lilikuwa haliepukiki kabisa!

2.Kwanini wataalam wetu walishindwa kutumia “case study” ya kilichotokea sehemu zingine Afrika katika kuanzisha tozo hii, ambako takwimu zinaonyesha kuwa moja ya mambo ambayo yalipingwa wazi wazi katika tozo hizi ni ukubwa wa tozo za miamala ya simu na kuwepo kwa “double taxation”.Mfano Nchini Malawi, wananchi walilamika kwa kuwepo kodi zaidi ya tatu kwenda kwa “users transfer & withdraw charges,agent withholding tax na kodi zingine kwa makampuni ya simu”!

Je,hatukupaswa kuja na version bora zaidi ya hii tuliyokuja nayo?je,kulikuwa na umuhimu wa kuunda kamati ya kumshauri Rais?,je,huku sio kukosa weledi kwa wataalam wetu?Kuna maswali mengi kuhusu utaalam na Weledi wa watu wetu”human resource capacity”.

Hakuna namna ambayo tungeweza kukwepa tozo hizi kwani kila Nchi barani Afrika kwa sasa inatoza watu wake katika naeneo haya ya “mobile money taxation”,suala la msingi ni je,tulipaswa kuja na utaratibu upi katika tozo hizi?!Mh Rais Jana kashasema kuwa hakuna namna kwani tozo lazima zitakuwepo tu hata baada ya kupokea repoti,swali lilikuwa je tozo hizi zinakuja katika”modality” ipi?.

4.Ni wazi kuwa Nchini, hatuna wataalam specifically wanajua”wabobezi” dhana nzima ya “digital economy”!Hii ni dhana pana katika uchumi wa kisasa na inapaswa kuangaliwa kwa jicho kubwa!Mfano Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya dola za kimarekani Trilioni 1.5+ zilikuwa zinazunguka katika uchumi wa Ivory Coast kupitia miamala ya simu kwa mwaka 2019.

Zaidi ya Dola za kimarekani Milioni 400+ zilikuwa zinazunguka katika miamala ya simu kwa mwaka 2019 Nchini Kongo!Uchumi wote huu unashindwaje kuutengenezea njia nzuri za kupata kodi tena bila kelele?

5.Je,wataalam wetu wamewahi kuishauri Serikali kwamba kabla ya kutaka kuanzisha tozo katika miamala ya simu japo la kwanza miaka mitano nyuma ilibidi tufanye “mobile money transaction deversification” Nchi nzima!lazima tulikuwa tuje na mpango mkakati kabambe wa “financial inclusion” kwa watu na taasisi zetu ili kuongeza wigo wa watumiaji wa huduma hii!”Wakulima,Shule,hospitali,sokoni,……”.

Unajua hii ingeleta nini?kwanza ingeongeza wigo wa watumiaji,watoaji wa huduma na automatically tungeongeza “tax base” kubwa na tungeweza kutoza tozo ndogo zaidi angalau hata asilimia 3 ya makato ya mapya kwa watumiaji hivyo wasingeona maumivu!Makato ya asilimia almost 30+ hayakuwa rafiki kwa Watanzania masikini na lazima yangeleta kelele!Simple economics!

USHAURI WANGU KWA SERIKALI YANGU YA CCM NI HUU HAPA!

1.Kuna fursa nyingi za kupata kodi na tozo katika uchumi digitali lakini lazima hatua za makusudi ya kutanua fursa ndani ya sekta hiyo zichukuliwe sasa!Mfano,Leo hii Serikali inaweza kuwawezesha vijana vijijini kupitia banki ya Kilimo kufungua shughuli za uwakala kwenye maeneo ya vijijini hivyo ikatengeneza ajira na kupata kodi toka kwenye miamala ya mawakala hao!Simple!

Banki yetu ya kilimo ya Tanzania “TADB” ingeweza kuelekezwa na Serikali kufungua dirisha dogo la mikopo kwa mawakala wa simu banki kwa ajili ya kuwaservice wakulima,wavuvi na wafugaji vijijini na kwa kufanya hivyo tungeweza kuutumia uchumi wa kidigitali vizuri zaidi!

2.Serikali inapaswa kusomesha wataalam zaidi katika sekta ya “digital economy” ili waweze kutufungulia fursa na kuishauri Serikali jinsi ya kutumia uchumi huu ambao unaonekana kuendelea kutengeneza fursa mkubwa katika masuala ya kodi,ajira na utengenezaji wa mitaji kwa vijana!Bahati mbaya vyuo vikuu vyetu navyo vimelala bado havijaona fursa hiyo ya masoko ya kielimu!

Serikali lazima iwe mbele katika “kupridict” fursa za mbele zitokanazo na uchumi wa kidigitali na Wizara husika inapaswa iwe na watu wenye akili kubwa ya kuona fursa hizi katika uchumi wa kisasa wa kidunia.

3.Ni wazi kuwa suala la tozo katika “Airtel” pia linaweza kuja kuleta kelele pindi litakapoanza kwahiyo Lazima hatua za haraka za kuweza kuliangalia suala hilo zichukuliwe sasa na ninaamini katika repoti atakayopokea Mh Rais suala hilo litakuwa limeangaliwa pia kwa mapana!

Wataalam wetu lazima wajue kuwa gharama ya maamuzi yao ya kisera na kisheria yana madhara ya moja kwa moja katika kutimiza malengo yetu kama Chama ya kuendelea kushika dola na hivyo Serikali ya CCM haitosita kuishauri Serikali kuwachukulia hatua watumishi wa umma ambao wanadhoofisha dhamira njema ya Serikali ya awamu ya sita!

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Serikali ya Wanafunzi Daruso -IJMC,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Vyuo Vikuu Vya Saut & Tumaini Iringa,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari -Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela mwaka 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %