

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 29,2021.
Gazeti la Habari leo la Jana lilibeba kichwa kidogo cha habari kuwa angalau asilimia 60 ya Watanzania wanatazamiwa kupokea chanjo ya uviko -19 baada ya huduma hiyo kuanza kutolewa rasmi jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa raia namba moja Nchini kuchanjwa rasmi.
Chanjo ya uviko 19 ingeweza kufikia hata asilimia 90+ ya uchanjwaji kwa Watanzania lakini tatizo kubwa kwa Serikali na wadau wengine tumewekeza kwenye “promotion” ya matumizi ya chanjo badala ya “education” kuhusu chanjo husika!Elimu ya chanjo haikuwa kubwa kwenye vyombo vya habari kiasi kwamba kumesababisha kuwepo kwa “denial” kutokana na kukosekana kwa “mental change” kwa Watanzania wengi!
Tunachopaswa kujua ni kwamba,kundi linalotaka chanjo hii, linahitaji chanjo kwa sababu linaofia kupata uviko- 19 na badae kukumbwa na vifo na hivyo hivyo kundi la wasiotaka chanjo pia linaofia kukubwa na kifo kutokana na kukosa elimu “information gap” ya chanjo za uviko -19.
Kwahiyo kwa kifupi,makundi yote mawili yapo katika mlengo wa kutetetea uhai zaidi kuliko kupingana na chanjo yenyewe ya uviko -19 ambayo imeendelea kutolewa duniani kote kwa sasa!
JE,MAISHA YA WATU HAWA HAYANA MAANA DHIDI YA MAISHA YETU?
1.Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais ndio Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama!
Nini maana ya kuwa Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama?kwa maana rahisi kabisa,huyu ndio (1) mlinzi namba moja wa mipaka ya Tanzania na maisha ya watanzania wote.Rais wa Nchi Amiri Jeshi Mkuu ana mamlaka kikatiba ya “kucommit” majeshi yake vitani wakati wowote atakapoona inafaa kwa ajili ya kulinda maisha ya watanzania na maslahi ya jumla ya Nchi na watu wake.
Mh.Rais Samia Suluhu Hassan, Jana ameongoza baadhi ya Watanzania kupokea chanjo ya uviko-19 ambayo inasemekana ina madhara kwa afya ya mwanadamu!Ni kichwa pekee yake mpaka sasa anayeweza kusema chanjo ya uviko 19 si salama kwa Watanzania!Ingewezekana vipi, Rais wa Nchi kujitoa sadaka dhidi ya maisha yake?
2.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikatiba ndio Mkuu wa shughuli zote za Serikali Bungeni!Waziri Mkuu pia ndio msimamizi Mkuu wa shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania!
Pamoja kuwa na majukumu hayo mazito ya kitaifa,Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, jana pia aliweza kupata chanjo yake ya Uviko 19 na kuwa “top second leader” kupata chanjo hiyo baada ya Mh Rais!Je,Chama chenu cha Mapinduzi ni vichaa kiasi gani kuruhusu haya yatokee?Mtanzania fungua minyororo yako ya ujinga nenda kapate chanjo haraka ikifika eneo lako!
3.Kikatiba,Mkuu wa JWTZ ndio Kiongozi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi na Usalama akiambatana Mkuu wa Jeshi la Polisi,Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa,Mkuu wa Jeshi la Magereza,Mkuu wa Jeshi la Uamiaji,Mkuu wa Jeshi la Zimamoto,Mkuu wa taasisi ya kupambana na Rushwa na Mkuu wa Uthibiti wa Madawa ya Kulevya wote wakifanya kazi za kiulinzi na Usalama!
Wote hao niliowataja juu,wanawajibu wa moja kwa moja wa kulinda maisha na mali za watanzania usiku na mchana lakini wajibu wao huo wa kulinda maisha ya watanzania uanza na wajibu wa kuyalinda maisha yao kwanza na ndio maana nyuma ya kivuli cha wakuu hawa utaona vijana wao”Body Guards” hivyo ulinzi wa maisha yao ndio kipaumbele cha kwanza kabla ya kulinda wengine!
Najiuliza Je,maisha ya Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa yanaweza yakawa hayana maana kuliko maisha yako?,maisha ya IGP Sirro hayana maana kuliko maisha yako?,Maisha ya CDF Mabeyo hayana maana kuliko maisha yako?,maisha ya Kamishina Generali Dkt Anna Makakala hayana maana kuliko maisha yako?,nakuachia maswali haya machache Mtanzania uyatafakari.
JE,WAJIBU WA VYOMBO VYA SIRI KATIKA MAAMUZI YENYE MASLAHI YA MAISHA YA WATU YANAKUWAJE?
Jukumu ya kwanza la Serikali yoyote duniani na mbinguni ni kulinda watu wake!Biblia takatifu inasema kuwa, Kristo Yesu aliwaambia wanafunzi wake”….kesheni na kuomba msije mkarubuniwa na shetani……”,hapa yesu kristo alikuwa anawalinda wanafunzi wake dhidi ya adui shetani!”protection role of the state”.








