George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 30,2021.
Nchi hii inakosa fedha nyingi hivyo kuendelea kujiita masikini kwa sababu ya kuwa na viongozi wasioweza kufikili nje ya box,hakuna tatizo lingine zaidi ya hilo!Kuna baadhi ya fursa ukiziona mpaka unashangaa na kujiuliza kwamba je,pana watu ambao hawapati usingizi kwa sababu ya kufikilia maendeleo ya watu wao?
Nchi hii tungekuwa na viongozi ambao angalau wanatumia masaa nane tu kati ya masaa kumi na mbili kufikilia wataifanyia nini Tanzania katika nafasi walizopo angalau tungepiga hatua kubwa katika kutafuta maendeleo ya watu!
Wiki Jana nilikuwa jiji Dar es salaam baada ya karibia miaka miwili ya kutokufika huko,wakati nakaribia makutano ya barabara ya Ubungo -Mwenge nakutana na mradi mkubwa wa ubungo interchange,kwa hakika jiji limebadilika sana!Hongera Serikali ya CCM kwa kazi nzuri hii ya hapa Ubungo!
Kesho yake nilikuwa namsindikiza jamaa yangu kuelekea uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julias Nyerere maeneo ya kipawa!Nashangazwa na mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja la juu”Flyover”!Kwa mara nyingine naona jiji limebadilika!Jamaa yangu akaendelea kuniambia kuwa kuna miradi mingine inaendelea katika maeneo ya makutano ya Mandela na Kilwa Road pale Chuo cha Uhasibu Kurasini,pia kuna miradi mingine maeneo ya moroco pamoja na kamata!very good!
Wakati miradi hii inatumia fedha nyingi tena za mikopo toka nje, je,Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji wanawaza nini jinsi ya kuisaidia Serikali kurudisha mikopo hiyo kupitia miradi hiyo mikubwa?mfano,mradi wa hayati Kijazi Ubungo Interchange unatokana na mkopo wa zaidi ya Tsh Bilioni 200+ kutoka Banki ya Dunia!Flyover ya Mfugale inakadiliwa kutumia zaidi ya Tsh Bilioni 188+!Tunazirudishaje fedha hizo za mikopo?
MKURUGENZI SMART LAZIMA LEO ANGEKUWA ANAPIGA HELA PALE NA KUONGEZA MAPATO YA NDANI”OWN SOURCE”.
1.Fly over ya Mfugale pale Tazara pekee ingeweza kumpatia Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke si chini ya Bilioni moja”1B Tsh” kwa mwaka!Je,Mkurugenzi hajui kuitumia flyover ile kutengeneza mapato?
Flyover ya Tazara kwa jina maarufu kwa “Mfugale”, kwa eneo ilipo automatically inavutia “potential & big advertisers” sababu tu ya uelekeo wake kwenda lango kuu la kuingia Nchini “Airport” kwa wageni wa aina mbalimbali!Tayari hiyo ni faida kimasoko!
Mkurugenzi kupitia afisa biashara wako unashindwaje kwenda kushawishi biashara zije “zistation” mabango yao ya matangazo pale Tazara?!Mfano,ATCL wangeweza kupamba kuta za Tazara Flyover na kukulipa fedha kibao kwa mwaka!
Hotel kubwa katikati ya jiji la Dar es salaam zingeweza kutundika mabango yao ya biashara na kukupa kodi kubwa kuliko wangebandika matangazo yao maeneo mengine ya jiji!Hivyo hivyo kwa makampuni mengine makubwa ya kibiashara!
Lakini kama sijakosea,mpaka leo sijaona bango la biashara la maana pale Mfugale Flyover!Naona ukuta wa Flyover zile una alama ya jina la Mfugale tuu!Je,ule ukuta ungepambwa na picha ya Ndege za Emirate tusingepata fedha kubwa zaidi?Tunakwama wapi viongozi wangu?
2.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo unakwama wapi?pale Ubungo interchange ungeweza kupata zaidi ya Bilioni mbili kwa mwaka kwa kuvutia advertisers tu!Ubungo kimara ndio lango kuu la usafiri wa barabara wa kuingia jiji kubwa la kibiashara ya Dar es salaam!
Kuta za Kijazi Interchange pale Ubungo zile zingeweza kukupa fedha kwa kuchapa matangazo ya biashara ya makampuni makubwa angalau kwa mwaka mmoja!Je,mafno,kampuni ya mabasi ya Sauli isingeweza kukupa fedha?Kampuni ya mabasi ya Shabib isingeweza kukupa fedha ya matangazo?
Barabara zilizopo ndani ya Kijazi -Ubungo interchange kwa kutumia tekinolojia ya kisasa pia zingeweza kukupa fedha kwa kuchapa matangazo juu ya barabara ile!Je,mabango ya Pepsi,coca cola,TBL je wasingekupa fedha pale?
Je,afisa biashara wa Manispaa hizo angalau wangekutana na wasaani na kuweza kuwashawishi kurekodi video au filamu zao je ,wasingepata fedhaa?Kwanini hatupo aggressive watumishi wa Umma?
Watendaji vijana wa Serikali lazima tuisaidie Serikali hii kuweza kukusanya mapato kwa kutumia elimu na ubunifu wetu!Haiwezekani Serikali ikawa imewekeza fedha zote hizo alafu kukawa hakuna “return on investment” wala hakuna “initiatives” za kutafuta fedha kwa ajili ya Wananchi wakati fursa zipo wazi!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Serikali ya Wanafunzi Daruso-IJMC,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Vyuo Vikuu vya Saut na Tumaini Iringa,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari- Maelezo,Ofisa Kadeti wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela mwaka 2020.