0 0
Read Time:3 Minute, 2 Second

Na Dr Yahya Msangi

Togo-West Africa 🌍

Katika sehemu ya pili nilieleza kuwa magaidi hutumia njia za halali na haramu kupata fedha. Pia hutumia njia za kizamani na za kisasa kupata pesa. Nilieleza pia katika kufanya hivi wanaweza kukuhusisha bila mwenyewe kujua na ukajikuta matatani kwa tuhuma ya ugaidi au kusaidia wengine wafanikishe ugaidi.

Hebu tuzipitie kwa kifupi hizi mbinu halali na zisizo halali, za kizamani na za kisasa:

  1. Njia halali
  • Michango (Donations)
  • Faida itokanayo na biashara halali na taasisi za kusaidia jamii -charity organizations)
  1. Njia haramu
  • Bishara haramu ya madawa ya kulevya (Drug Trade)
  • Biashara haraùu ya silaha ikiwa ni pamoja na silaha za maangamizi (Weapons of Mass Destruction – WMD)
  • Utapeli, kugushi (Fraud)
  • Utekaji kwa nia ya kupewa fedha (Kidnapping for ransom)
  • Utishaji kwa nia ya kupata fedha (Extortation)
  • Wizi -theft)

Njia hizi wanatekeleza kwa ùtindo wa kizamani na mtindo mpya. Miaka ya hivi karibuni magaidi yamejikita zaidi kwenye kutumia njia za kisasa kujipatia fedha kwa kutumia:

  1. Social media haswa zifuatazo: YouTube, LinkedIn, Instagram Facebook, Twitter, RenRen, Sina na Weibo. Najua nyingine huzijui!

Social media zmewapa faida kubwa kwa kuwa zinawezesha magaidi kuwafikia mabilioni ya watu kwa haraka na kwa gharama nafuu. Ni rahisi na salama kwao kupata hela kupitia social media kuliko kwa mfano kuteka watu au mtu. Kueka mtu kunahitaji kumfuata, kumhifadhi, n.k. Ni hatari kwao. Mara nyingi wasipolipwa inabidi waue na hivyo kuongeza kosa!

Kupitia social media magaidi wamefanikiwa kuhusisha watu ambao hawana habari kuwa rafiki au group alilojiunga asili ni ugaidi!

Hapa ndio wengi wenu mnajikuta mnwezesha ugaidi bila kujijua!

Mifano:

  • Magaidi wanaweza kumtumia mwenzao aanzishe ukurusa au group na ajidai kuna mgonjwa anatakiwa kuchangia. Na wewe kwa kujifanya umeguswa unaweza kuchangia ukidhani unasaidia mgonjwa! Siku wenye kazi zao wakifuatilia na kukuta wewe ni mmoja wa uliochangia wanakuweka kwenye uchunguzi! Binafsi utadhani ulichangia mgonjwa kumbe uliwezesha tukio la ugaidi lilioua watu!
  • Magaidi wanaweza kuanzisha charity organization na wakaomba kamchango kadogo ka dola 1! Kwenye tovuti yao wataonyesha wanasaidia maalbino, watoto wa mitaani, wahanga wa UKIMWI, n.k. Wewe utaona dola 1 ni ndogo na utachangia ukiamini unasaidia maalbino! Hela hivyo inaweza kutumika kununua mlipuko wa kwenda kuetekelza ugaidi. Wanaweza kuita charity yao Christian au Islamic au Hindu bla bla bla ili uvutiwe!

Magaidi wanajua kwa mfano Facebook ina watumiaji bilioni 1 (by year 2018), Twitter million 500 (by 2018) na RenREn ilikuwa na million 160! Ikiwa asilimia 5 tu watachangia dola 1 ni mabilioni watajipatia bila wachangiaji kustuka!

Magaidi pia wanajua ukweli huu:

  1. Ilichukua teknolojia ya radio miaka 38 kupata wasikilizaji milioni 50
  2. Ilichukua tech ya TV miaka 13 kupata watazamaji milioni 50
  3. Ilichukua internet miaka 4 kufikia watumiaji milioni 50

LAKINI
Ilichukua facebook miezi 9 tu kupata watumiaji milioni 100!

Magaidi hawakutaka fursa hii ipite bila kuitumia!
Matumizi ya social media yameongeza ugumu wa vyombo vya kiusalama vya kitaifa na kimataifa kuzuia magaidi wasipate fedha za kuendesha shughuli zao za kigaidi.

Makala ijayo nitaelezea namna mbalimbali ambazo magaidi hutumia social media. Ila inafaa ukumbuke kuwa magaidi hawatumii social media kwa kupata fedha peke yake. Huitumia kupata wanachama (recruitment), kununua silaha na vifaa watakavyo, kutolea mafunzo ya kigaidi, kuwasiliana, kupanga shambulizi, kuhamasisha (radicalization), n.k. Pia makala ijayo nitaelezea jinsi magaidi wanavyofanikisha usafirishaji na utakasaji fedha zao. Ujio wa cryptocurrency umewapa njia nyingine mpya ya kutakasa na kuficha fedha zao. Nitaeleza cryptocurrency, ziko aina ngapi kwa sasa ni nini na inafanyaje kazi. Bwana Lema alihimiza Tanzania ianze kuitumia cryptocurrency!!!! Nitaeleza ni kwa nini Tanzania isikurupuke na ipuuze ushauri wa Bwana Lema. Ni ushauri wenye harufu ya kigaidi!

ATUTELER A TOUS!

ONYO: NI MARUFUKU KUKOPI MAKALA HIZI NA KUJIMILIKISHA.Nimeona vibaka fulani wanakopi na kushare kana kwamba makala hizi ni zao! Block inafuata!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %