Na H.Mkali
mkali@live.co.uk
Mwandishi wetu nguli msomi,mchambuzi wa masuala ya kidiplomasia na siasa za Kimataifa ,ameandika katika kuwaza kwake kwa sauti kuhusu taarifa hii inayosema kuwa kampuni ya Winshear Gold imeshinda kesi ya madai dhidi ya Serikali ya Tanzania,hivyo serikali inatakiwa kulipa kiasi Cha dollar za Canada C$124,781,945.

Kwa kigezo gani hiyo kampuni ilifikia hicho kiwango
Hiyo mahakama iliyokubali hayo madai nayo ni mahakama ya kipuuzi kweli kweli.
Kwa nini hawa washenzi ( watovu wa ustaarabu) hawakufaili haya madai yao enzi za Magufuli? Kwa sababu walijua kuwa Magufuli hakuwa “jelly fish.“
Na haya yanaweza kuwa yametokana na Serikali yetu kuwaonyesha mabeberu udhaifu wetu usiokuwa na kiasi, kadri au wastani.
Ni sisi wenyewe tumewashawishi hawa washenzi wadiriki kutufanyia mambo kama haya.
Ushauri Wangu
- Serikali yetu ipuuze kabisa hayo madai;
- Tanzania ijitoe kwenye ISDS Investor-State Dispute Settlement mechanism. Nimeyasema haya tangu enzi za serikali ya awamu ya tatu.
Kesi zote Kati yetu na Mwekezaji zisikilizwe kwenye mahakama zetu za ndani. Na asiyelitaka hilo na asije kuwekeza Tanzania.
Nchi kama Brazil hazipo kwenye mikataba ya ISDS na wala haina ukame wa Wawekezaji wa Nje.
Kwa wingi wa raslimali tulizonazo, Ulimwengu unaijitaji Tanzania zaidi kuliko Tanzania inavyouhitaji Ulimwengu. Lakini wengi wa viongozi wetu wamekuwa ni vipofu (hawauoni au hawataki kuufungulia macho ukweli huu.
This the real tragedy here.
mkali@live.co.uk
26/08/2021.








