

George Michael Uledi.
Kyela Mbeya
August 27,2021.
Ni wazi kuwa uchunguzi wa tukio la “Gunshoot” lilofanywa na kijana anayetambulishwa kwa jina la Hamza juzi katika maeneo ya ubalozi wa Ufaransa unaweza usiwe mwepesi kwa vyombo vya uchunguzi na unapaswa kuwa endelefu hata baada ya kutolewa kwa repoti ya awali.Sababu kubwa ya ugumu wa uchunguzi huo ni kukosekana kwa mashahidi muhimu wa tukio ilo kwa maana ya Polisi na mhusika aliyetekeleza mauaji hayo!
Watalaam wa masuala ya uchunguzi nadhani wanajua kazi ngumu inayowakabili kuhusu tukio husika hasa katika kujua chanzo cha mauaji hayo ya juzi!”Shooting incident analysis”.Pamoja na yote hayo bado nina imani na taasisi zetu za uchunguzi kwamba zitaenda kuleta ukweli kuhusu tukio husika.
MASWALI PASUA KICHWA YA KUJIBU KUHUSU KIJANA “HAMZA”.
1.Hamza aliweza kujipambanua kuwa yeye sio mgeni wa kutumia silaha vita kwa jinsi alivyokuwa anajua “attacking movements”!Hamza alionekana wazi kujua jinsi ya kumshambulia adui na kutafuta maficho kwa usahihi mkubwa”cover”.
Uwenda kijana Hamza kuna sehemu aliwahi kupata mafunzo haya kwani sio kawaida sana kwa raia wa kawaida kuweza kufanya mambo ambayo kijana huyu alikuwa anayafanya kupitia picha mbalimbali za tukio husika tena kwa usahihi mkubwa!Panahitajika uchunguzi wa kina kujua Hamza ni nani?
2.Suala la pili ni jinsi Kijana yule alivyokuwa “confortable” na silaha kubwa!Kitendo chake cha kujua”kukoki” na kupiga silaha bila wasiwasi sio cha kuchukulia poa!
Kiutalaam,mtu ambaye hajawahi kutumia silaha kubwa,tulitegemea angefanya makosa katika matumizi ya risasi”ammunition management”.Hamza angekuwa sio mtaalam wa silaha ni lazima angepiga”rapid ammunition” kitu ambacho kingemfanya aishiwe na risasi mapema hivyo Polisi kummaliza mapema!
Lkn kijana Hamza hakuonekana akipiga “rapid ammunition” bila sababu,alikuwa anapiga style hiyo pale alipoona “target” tu!Hamza anayajua wapi yote haya?!Tunahitaji utulivu na taratibu kumjua Kijana huyu kabla ya tukio alikuwa na konection na nani na wapi?
3.Kijana Hamza anaonekana kwenye picha kwamba ni mtu anayejua kuchukua tahadhari kabla ajaanza kuondoka kutoka “cover” moja kwenda “cover” nyingine.Kabla hajaondoka sehemu aliyosimama, aliweza kuangalia kushoto na kulia zaidi ya mara mbili ili kuweza kujiridhisha kuhusu uwepo wa adui!Hii sio kawaida kwa mtu ambaye hajawahi kuonja uwanja wa medani!
Ukimwangalia kwa makini unaona jinsi alivyokuwa mzuri kwenye “weapon positioning” kwani alipoanza “kumove” aliweza kuishika silaha kwa usahihi na kwa utulivu mkubwa”hakuwa na mtele”.Je,Kijana Hamza ni nani?Kijana huyu anafikilisha sana!
4.Kijana Hamza anaonekana kafundishwa na pia anajua somo la kumpokonya adui silaha na kwa kuthibitisha hilo inasemekana kuwa aliweza kutumia silaha yake ndogo”pistol” kupokonya silaha kubwa ya askari Polisi kwa ajili ya kuendeleza mapambano na Askari yoyote atakayekuja mbele yake!
Katika hali ya kawaida, Kijana huyu Hamza angekuwa sio mtaalam wa mambo ya medani, lazima angeendelea kutumia pisto yake kuendeleza mashambulizi dhidi ya Askari lakini akaenda mbali kwa kwenda kupora silaha kubwa kwa ajili ya kuendeleza mapambano!
5.Kwanini Kijana Hamza hakuwaza “kuwithdraw” baada ya kuwaua Askari wale?kwanini alitaka kuendelea kupambana na Askari wengine?Alikuwa anataka nini?
Hii ishara ya awali kuwa Kijana huyu alikuwa na dhamira ya muda mrefu na sio tukio la siku moja!Ujasiri ule hauwezi kuupata ndani ya masaa au dakika kadhaa!Haiwezekani!
KIJANA “HAMZA” ANATUPA SOMO GANI?
1.Kuna wakina Hamza wengi mitaani kwetu na tusipoanza kuwathibiti mapema tunaweza kupata madhara makubwa!
2.Askari wetu lazima wachukua tahadhari sana na mapema za kabla ya kuanza kujibizana na mtu yoyote!Mkague na pokonya silaha yake mtu yoyote ambaye unafanya nae au unataka kufanya nae mahojiano!Hii itasaidia sana kuepusha maafa!
3.Kuna umuhimu mkubwa sasa utambulisho wa Raia yoyote kupitia kitambulisho chake basi tungeweza kuweka alama inayomtambulisha mhusika kwamba je, anajua kutumia silaha au lah!Hii ingesaidia sana Askari na watu wengine kuchukua tahadhali hasa wanapowahoji wateja wao!
Mfano,Askari wetu wa Usalama barabarani ambao mara nyingi wanakwaruzana na madereva wanaweza kuingia katika matatizo makubwa siku moja!Askari anapaswa kumjua anayemuhoji kupitia “driving kard” ili kujua jinsi ya kudeal nae kwa maana ya tahadhali!
Kwa ufupi,tukio la Kijana Hamza linafikilisha sana na majibu yake yanaweza yasiwe mepesi sana!Nashauri uchunguzi wa muda mrefu zaidi unahitajika ili kuweza “kupridict” matukio mengine yanayoweza kuja na kuyathibiti!
Mwandishi ni Kijana wa CCM,Rais wa zamani Serikali ya Wanafunzi Daruso -IJMC,Ofisa wa zamani, Idara ya Habari -Maelezo,Ofisa Mwanafuzi wa zamani, Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.