
Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo ambae kwa sasa ni bingwa wa Africa alijibu taarifa ya kumtaka kupambana na mwana masumbwi Dula Kiduku kwa ofa ya gari iliyotangazwa na Mbunge Babu Tale. Hassan Mwakinyo ambae amejizolea sifa nyingi na wapenzi wengi nchini baada ya kushinda mapambano yote kwa sasa ,alijibu mualiko huo akiwa nyumbani kwake alipotemmbelea na Wana Habari.
“Kama wanaweza, bondia yeyote anayetaka kupigana na mimi Tanzania, wamtengeneze afike nyota nne, yani nijue bingwa anapigana na bingwa, sio bingwa anapigana na mbeba matofali, au bingwa anapigana na mbeba mizigo, hiyo ni kashfa, hizo ni dharau.
“Yeye anajua umhimu wa branding ni nini, ndio maana kuna wakati akina @babutale Babu Tale hawamuingizi @diamondplatnumz kwenye vita na wasanii wa chini yake sababu wanaona wanamshusha, kwa nini mimi ananichukulia poa? Sio sawa. I promise nitafika World Champion, na Babu Tale nitamnunulia V8 tatu na sitohitaji chochote kutoka kwake – Bondia Mwakinyo









