0 0
Read Time:1 Minute, 5 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
August 28,2021.

Hamza Mohamed Kijana aliyetekeleza mauaji ya askari Polisi maeneo ya ubalozi wa ufaransa majuzi inawezekana akawa “chambo”.?

Je, kijana Hamza ametumika”kulianzisha” ili kupata “justification” ya kitakachokuja mbele!Hii Naomba iwe “alart” kwa vyombo vyetu kwamba inawezekana kijana Hamza atakuja tena!

Inawezekana Tanzania tunatafutwa na watu fulani lazima tuchukue tahadhali mapema!Wakati huu ISIS kule Msumbiji katika Jimbo la Delgado wanafulumushwa lakini hatujui wameelekea wapi?Tanzania au Kwingineko!

Wajibu wangu ni kunusa na kushauri!Isije ikawa kijana Hamza katumika kama “Chambo” cha kulianzisha!Kwanini leo?IGP Sirro wiki kadhaa alikaririwa kusema kwamba wale wa kibiti wanaweza wakawa wameanza tena!Vijana wa IGP wamenusa hatari hiyo!

Mzee wangu IGP, Sirro Je,tunatafutwa?na nani?kwanini?Nahisi kijana Hamza katumwa kulianzisha “dume” ili waseme”tutalipiza”?

Nawasihi Watanzania kwamba ulinzi wa Taifa ni wetu wote,ukiona tukio au watu aina ya Hamza haraka toa taarifa katika vyombo vya dola!Pamoja tutashinda!

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro

Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Serikali ya Wanafunzi Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani Idara ya Habari – Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %