0 0
Read Time:2 Minute, 57 Second

George Michael Uledi!
Kyela,Mbeya!

Ni wazi kuwa upinzani Nchini Tanzania unahitaji miaka zaidi ya kumi ya kujiandaa ili angalau kuweza kuja kushindana na Chama cha mapinduzi ambacho kimeonekana kuwa na “njaa” ya kuendelea kushika dola!

Chama chochote kinachotaka kuendelea kushika dola lazima kiwe na “njaa” na wivu wa kutaka kushikilia dola husika!CCM ni wazi kuwa bado inaonekana ina “njaa” ya kuendelea na kutaka kuishika dola na kuwatumikia Wananchi wa Tanzania!

“Njaa” hii ya CCM ya kutaka kuendelea kushika dola inathibitishwa na mipango ya wazi ya kimkakati ambayo imekuwa ikifanywa na CCM kupitia Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan!

Itakuwa ni ndoto za mchana kuwaza kuishinda CCM hii,CCM hii yenye malengo ya muda mrefu ya miaka zaidi ya mia moja mbele!Upinzani angalau unahitaji miaka zaidi ya kumi ya kujiandaa ili kuweza kushindana na CCM .

KWANINI NI NGUMU KUISHINDA CCM KWA SASA?

CCM imejengwa katika nguzo kuu tatu ambazo unahitaji uwe na malengo marefu, mbinu mkakati na muda wa kutosha wa kuweza kuzibomoa!Ni kujidanganya kudhani kwamba CCM unaweza kuishinda kwa kutumia mipango zimamoto hii ya vyama vya upinzani!

1.Sera bora za CCM ndio roho ya CCM ilipo!CCM imeweza kujipambanua katika kutengeneza sera ambazo zinajibu mahitaji ya sasa na ya mbele ya Watanzania!

Kwa mfano,ukisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 mpaka 2025 kwenye kitabu cha ni kurasa 307 wazi kuwa unaweza kujua Tanzania baada ya mwaka 2025 inaweza ikawaje!Maono hayo makubwa ndio ambayo yanaifanya CCM kuendelea kuaminiwa na Watanzania!

Ili Chama cha siasa kuweza kupata kura lazima kiwe na uwezo wa kuwatamanisha wapiga kura wake mambo yanayogusa maisha yao ya kila siku!CCM imekuwa na uwezo mkubwa wa kuwatamanisha watanzania hivyo kujenga imani ya kufikia ustawi wao!

2.CCM imekuwa ikijivunia uwepo wa hazina kubwa ya wanachama wenye kila aina ya weledi na taaluma!Mchanganyiko huo wa Wanachama wa CCM wenye kila aina ya ujuzi ndio unaifanya CCM kuendelea kuaminiwa na Watanzania!

CCM uzalisha viongozi bora kutokana na kuwa na kapu kubwa la rasilimali watu kutoka kada mbalimbali za maisha hivyo kukifanya kuwa Chama chenye kuheshimika na kuaminika zaidi!

Labda CCM ndio Chama pekee ambacho kinaweza leo hii kikavunja Serikali yote na Kesho kuja na sura mpya kabisa tofauti na Chama kingine chochote Nchini!

3.Nguzo ya mwisho ya CCM ni uwezo wake wa kuisimamia Serikali yake katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama.CCM imeweza kuwa Chama ambacho kimeweza sana kuisimamia Serikali hasa katika masuala ya kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania!

Kwa mujibu wa repoti ya juzi ya TRA,robo tatu ya kwanza ya mwaka 2021/2022,TRA imeweza kukusanya kiasi cha Trilioni 5+ zaidi ya kile kilichokusanywa kipindi kama hiki mwaka uliopita!

Uwezo huu wa Serikali wa kukusanya kodi unawezesha urahisi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 mpaka 2025 pamoja na mipango mingine ya kitaifa!

Ni wazi kuwa upinzani unahitaji muda zaidi wa kuweza kushindana na CCM na kama CCM itaendelea kuwa na ndoto,maono na uthubutu wa kufanya mambo makubwa basi itawachukua muda mrefu sana wapinzani Nchini kuja kuiondoa CCM madarakani!

Mwandishi ni Mhadhiri wa zamani Tumaini na Saut University,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha.

+255746726484
+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %