

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 8,2021.
Ni wazi kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Ushetu wilayani kahama mkoani Shinyanga kupitia tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Charahani, atashinda uchaguzi huo asubuhi na mapema kesho!
Kuna sababu kubwa mbili za kuifanya CCM kushinda uchaguzi huo asubuhi na mapema kesho (i)uwepo na CCM imara ambayo kila siku ineendelea kujitengenezea mizizi katika ngazi ya mashina na matawi huku(ii) vyama vya wapinzani vikitumia nguvu kubwa katika kutafuta katiba mpya ambayo pia ajenda hiyo imeonekana kupuuzwa na wananchi hasa wale waishio vijijini!
Baada ya CCM kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliopita,vyama vya upinzani havijawahi hata kufanya tathimini ya nini kiliwatokea mpaka wakashindwa vibaya na CCM badala yake vilitumia muda mwingi kulaumu kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki bila kuwa na ushahidi wa hoja hiyo!
CCM ina utaratibu imara wa kufanya tathimini baada ya uchaguzi kupitia vikao vyake mbalimbali hata kama watakuwa wameshinda au wameshindwa Uchaguzi husika!
Utaratibu huu unaendelea kuwapa CCM faida ya kuendelea kushinda chaguzi katika kila jimbo kwani tathimini hizi ukisaidia Chama katika(i)kujua madhaifu na ubora wao(ii)kujua matatizo ya wananchi wa jimbo husika(iii)kuaanda mipango utekelezaji ya matatizo hayo ili kujenga uhalali kwa wananchi katika chaguzi zijazo!
KWANINI CCM ITASHINDA ASUBUHI NA MAPEMA KESHO JIMBO LA USHETU ?
Nguvu ya CCM katika kanda ya Ziwa uenda ikaendelea kuongezeka zaidi kutokana na sababu mbalimbali wakati huo huo ushawishi wa vyama vya upinzani katika kanda hiyo hiyo umekuwa ukipungua kwa kasi kubwa!Sababu kubwa hizi hapa tano(5) zinaifanya CCM kuwa na uhakika zaidi wa kushinda uchaguzi huo kesho!
1.Ujenzi wa mradi mkubwa wa SGR kutoka Dar es salaam kuelekea kanda ya ziwa kunaipa CCM uhalali na kuaminika zaidi kwa wananchi wa kanda husika likiwemo Jimbo la Ushetu lenyewe!
Kete hii pekee yake inaweza kuipa ushindi wa asilimia zaidi ya 60 kwa Chama cha mapinduzi!Mikoa ya kanda ya ziwa hasa Shinyanga,Geita, na Mwanza kwa sasa inaunganishwa na usafiri wa anga,maji na reli wa kisasa!kazi hizi za utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM ndio kunaifanya kazi iwe rahisi mno kesho kwa Ndugu Charahani!
2.Mafanikio makubwa ya uwepo wa Halmashauri mpya na jimbo jipya la uchaguzi ni kazi nzuri ya Chama cha mapinduzi ambapo mwaka 2012, Serikali ya CCM kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi wa Ushetu,iliamua kugawa wilaya ya Kahama katika majimbo matatu ya Kahama,Msalala na Ushetu!Ni wazi kuwa wananchi wa Ushetu hawana mbadala wa CCM kutokana na kusogezewa huduma karibu yao zaidi na wananchi wanaona kwamba Mgombea wa CCM pekee ndio anaweza kuendeleza mazuri haya!
3.Ni wazi kuwa katika Uchaguzi wa kesho,CCM inakutana na utitiri wa wapinzani wasio na madhara wala ushawishi kwa wana Ushetu kwa sababu moja tu kwamba mpaka sasa zaidi ya vyama 16 vimejitokeza kuchukua fomu za uteuzi wa kugombea Ubunge vikiwepo chama cha CHAUMA,ADC,SAU,NRA,ACT,TLP,UMD,AAFP,CCK na vinginevyo!
Ni wazi kuwa mgombea wa CCM Ndugu Immanuel Charahani anaweza kupata ushindi wa juu ya asilimia 90 kesho hivyo kuendeleza utawala wa CCM katika kanda ya ziwa!
4.Sababu nyingine ya uwepo wa ushindi wa asubuhi kesho kwa CCM ni kuaminika kwa mbunge aliyepita marehemu Elias Kwandikwa kwa wana Ushetu!Heshima kubwa ya marehemu Elias Kwandikwa inatokana na uwepo wa miradi mikubwa ya maendeleo ndani ya muda mfupi ambayo ni kazi nzuri ya Serikali ya CCM chini Rais Samia Suluhu Hassan!Uwepo wa miradi mikubwa ya maji,afya na barabara ndani ya kipindi kifupi tangu kuzaliwa kwa Jimbo hilo kunaipa CCM asilimia zaidi ya 90 ya kushinda kesho!
5.Principle ya ushindi wa CCM mahara popote ni matumizi ya “sheria ya ushindi vita” inayoitwa “Concentration of forces”!Dhana hii ya vita inasema hili uweze kumthibiti adui katika uwanja wa medani lazima umshambulie kwa(i) nguvu zako zote (ii)akili yako yote(iii) kwa silaha zako zote!
CCM katika kuutafuta ushindi hawajawahi kumpuuza adui hata siku moja!Wakati leo wanafunga pazia la kampeni Ushetu,Waziri Mkuu mstaafu Mh. Mizengo Kayanda Pinda atakuwepo!Uwenda leo Mzee huyu ndio anaenda kuwasha mitambo kwa ajili ya ushindi wa CCM kesho!
Nasubili kuona aibu kubwa kesho,nasubili kuona Mh.Emmauel Charahani akibebwa juu juu kushangilia ushindi kesho,nasubili kuona Spika Job Ndugai akipata mteja mwingine wa kijani bungeni!
Zaidi nasubili kuona ushindi mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan mwaka wa 2025.Naiona Tanzania mpya ya kesho,ileeee!

Mwandishi ni mchambuzi wa siasa,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri wa zamani,vyuo vikuu vya Saut -Tabora na Tumaini Iringa na Mtia nia wa CCM Jimbo la Kyela 2020.
+255746726484.
+255784159968.








