0 0
Read Time:1 Minute, 5 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 4,2021.

Nini kimesitisha safari za treni kati ya dar-moshi-arusha baada ya Serikali ya awamu ya tano kuifufua?kabla ya mwaka mmoja ya kuanza kufanya kazi baada ya kukwama miaka nenda rudi?nini kinaendelea?

Reli ile ilikuwa inaanza kupata faida kubwa baada ya watu wengi wa kaskazini kuanza kuitumia katika kusafiri na usafirishaji wa mizigo?je,Serikali yangu ya CCM inasemaje?je,hii haiwezi kutupotezea wafuasi wetu katika mikoa husika?

Ni wazi kuwa mradi ule wa reli ulikuwa ni “bakora” kwa ngome ya upinzani ambayo mizizi yake ipo kaskazini!je,hii haiwezi kutupotezea ushawishi wetu katika mikoa husika?

Watendaji wa Serikali wanaipa kazi kubwa CCM ya kurudisha ngome tuliyoiteka ya kaskazini!haya ni Mambo ambayo yanaweza kutupotezea ushawishi kwa watu watu basi kama wakubwa wanasikia watusaidie kurudisha huduma katika eneo husika kwa haraka hata mara moja kwa wiki basi kwa kuanzia.

Ni bora SGR isimame lakini reli hii iliyoanza kutoa huduma na kutembea baada ya kufufuliwa na Serikali ya awamu ya tano, eti leo haifanyi kazi tena?Mbona watendaji serikalini tunataka kumbebesha mzigo Mama yetu?Hii kazi Rais Samia na JPM walishaifanya,nini kinaendelea kule kaskazini?Masanja Kadogosa?unatwambia nini?

Chama changu CCM tunapaswa kuwa wakali kwani huu ni mzigo kwetu hatupaswi kukaa kimya katika hili!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %