
Na Mwandishi wetu WU®
Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi amekutana na ujumbe wa Madaktari kutoka ‘Hackland University Hospital’ ya nchini Norway, ambao wamekuwa wakisaidia Hospital ya Wagonjwa wa Akili Kidongo chekundu katika nyanja za miundombinu, vifaa pamoja na mafunzo na hivyo akatumia fursa hiyo kuomba kupanua wigo wa misaada yao.
Amesema kazi ya kuandaa miundo mbinu ya Afya ni jukumu la Serikali, lakini kutokana na mahitaji makubwa katika sekta hiyo ya Afya, Serikali inashajiisha wafadhili wa ndani na nje ya nchi pamoja na sekta binafsi kusaidia.
Amewapongeza madaktari hao kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya, sambamba na kuwataka kuwa Mabalozi kushajiisha taasisi nyengine kutuma misaada yao kwa Zanzibar.










