0 0
Read Time:3 Minute, 37 Second

Watakaopata mimba ruksa kurudi shuleni” Prof. Ndalichako

George Michael Uledi.
Kyela, Mbeya.
Nov 25,2021.

Ni kama “Mwamba” hayati John Joseph Pombe Magufuli unaweza kusema alikuwa na kajicho kaunabii fulani ndani ya mboni yake hasa pale analiposimama na kusisitiza zaidi ya mara tano katika majukwaa tofauti ya kisiasa na kusema, nanukuu”โ€ฆ.watanzania mtanikumbuka na sio kwa mabaya hila kwa mazuri..”.

Wakati mwingine unajiuliza maswali mengi kidogo, kuwa Je, John Magufuli “Mwamba” alipata wapi confidence ya kuyatamka maneno haya hata kabla hajafariki dunia?.

Je,Chuma hayati JPM alikuwa anajua kuwa baada ya kifo chake kutakuja tokea kizazi kama cha kina PROFESA Joyce Ndalichako ambaye ni Mwalimu kitaaluma ambaye unaweza kusema ameshindwa acha kuusimamia Uprofesa wake bali kashindwa angalau kusimamia maadili ya Taifa pamoja na maadili ya taaluma yake mwenyewe ya ualimu.Niliwahi kuandika,”Nchi ya Drama Imeshaanza”.

Wanasiasa wetu hawa tena wasomi wengine ngazi ya uprofesa badala ya kumshauri vizuri Mama huyu msikivu, yaliyo mema kwa mustakabali wa Mila na desturi za Taifa hili nao wameanza kuwaza jinsi ya kuimarisha uteuzi wao kwa Mh. Mama Samia Hassan kuelekea mwaka wa uchaguzi wa 2025 na kusahau kabisa wajibu wao wa kwa Taifa hili!

Makosa makubwa tunayoyafanya leo kama Taifa, kwa kuamua kuruhusu mambo yasiyo na tija kwa UTAMADUNI wetu kwa kisingizio cha kuutafuta ukombozi wa mwanamke tu, gharama yake inaweza isibebwe na Serikali ya awamu hii ya sita, LAKINI inaweza ikaja kubebwa na Taifa zima!Intervations hizi za kiwanaharakati tunazozifanya leo ndani ya Taifa letu, gharama yake ni nzito mno kuliko gharama ambazo wanazibeba Mama zetu na wanawake wa kitanzania leo dhidi ya mfumo dume huu!

Waziri wa elimu Prof. Joyce Ndalichako

NINI WANAWAKE WA KITANZANIA WANAPASWA KUJUA KUHUSU HIKI WANACHODHANI NI UKOMBOZI KWAO LEO?

1.Ukombozi wowote wa binadamu yoyote duniani, uwe wa ukombozi wa kiuchumi,kiutamaduni,kisiasa na hata kijinsia ” it is based on a gradual process changeโ€ฆ” na sio “event”,kwa maana ya sio tukio!

2.Kama Mama zetu na jamii ya wanawake wa Kitanzania kwa ujumla, wanadhani au watadhani kuwa, ukombozi wao dhidi ya kile wanachoita mfumo dume katika jamii yetu ya Tanzania na Afrika, utapatikana kwa kufanya “matamko” na “matukio” basi wanajidanganya sana!

3.Yale yote yote yanayofanyika sasa, baada ya awamu hii yanaaenda/yatakwenda baadae kuzalisha kitu kipya kwa jina la “gender class struggle”, mpya kabisa ya wanaume dhidi ya wanawake kuanzia majumbani mpaka Taifani.Kwa bahati mbaya sana “Gender Class struggle” hii itakayokuja ya wanaume dhidi ya wanawake, itakuja kuwa “more coesive ” kwa wanawake zaidi, kuliko hii iliyopo sasa sababu kujikwamua huku kwa mwanamke kutoka katika mfumo dume,wanaume wengi watadhani/wanadhani, kunaendana na matukio ya kupoteza utamaduni,mira na ustaarabu wetu kama Taifa!

4.Ni wazi kuwa huko tuendako mbeleni, idadi ya wanawake katika uchaguzi wa mwaka 2025 ndani ya CCM itakuwa kubwa kuliko kipindi chochote katika historia ya Chama hicho!Hii ina maana gani?Natabiri uwepo wa mipasuko kwa kiasi fulani ndani ya CCM kutokana na upepo huu!Kama CCM haitoliona Hilo sasa,gharama yake kwa afya ya ushindi wa CCM itakuja kuonekana!

Mipasuko hii ya ki “gender powers struggle”haitoishia ndani ya vyama vya siasa tu bali itaenda mbali zaidi mpaka kwenye siasa za vyama kwa vyama hivyo kuweza kuleta mpasuko mkubwa wa kijinsia na Taifa kwa ujumla!

5.Serikali yangu ya CCM inapaswa kuwa makini mno na hii ” evental gender transformation” tunayoitekeleza!Hii sio wazo baya LAKINI inaonekana approach yake inaweza kuleta madhara makubwa Kwa Chama changu!

kamwe wanaccm tusidhani kwamba “gender impowerment ” ni tukio”event”ambalo linaweza kuwa “achieved” ndani ya miaka kumi!Lazima tujue kuwa” this is a gradual process which goes with natural factors such as time, interactions & social exposure”.

Chama changu tawala yaani CCM, kikiendelea na njia hii kwa kuwachia watu”individuals”, waamue mustakabali wa Nchi bila kuangalia madhara mapana kwa maslahi ya Taifa dhidi ya maslahi ya makundi, basi tumekwisha!

Eti Profesa JOyce NDALICHAKO kwa maana ya Serikali, inasemaa,”โ€ฆwanawake + watoto wa kike wote walipata mimba wakiwa shuleni,itakuwa ruksa kurudi KUENDELEA na masomo yaoโ€ฆ..”Dah,kila mtu mtaani anachekaaaaaaaa!

Ahadi moja wapo ya mwanaTanu iliwahi kusema”โ€ฆnitasema kweli daima fitina kwangu ni mwikoโ€ฆ”.

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Chuo Kikuu vya Saut na Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %