0 0
Read Time:4 Minute, 14 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 28,2021.

WU®

Wakati TAIFA la Tanzania linatimiza angalau miaka 60 ya uhuru wake ifikapo Desemba 9,2021,chama cha mapinduzi na serikali yake chini ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan wanaweza kusimama na kupiga kifua jinsi ambavyo sekta ya madini ilivyoweza kupata mafanikio ya kutosha ndani ya miaka angalau sita tu.

Kutokea kwenye lindi kubwa ya sintofahamu na malalamiko mengi kutoka kwa Wananchi kuhusu serikali kuibiwa katika sekta husika na wawekezaji,ni serikali ya awamu ya tano chini ya watu wawili shupavu, hayati mwamba John Pombe Magufuli na makamu wake Rais wa sasa,Mh Samia Suluhu Hassan, waliweza kupindua meza na kuyafanya madini kuwa neema kwa Taifa badala ya kuwa laana!

Ni siku ya jumatatu mchana ya tarehe July 10,2017 historia mpya iliweza kuandikwa katika Taifa kubwa kupit yote Afrika mashariki yaani Tanzania!Rais wa wakati huo John Pombe Magufuli na makamu wake Samia Suluhu Hassan historia itawakumbuka!

Kijana mdogo kutoka katika jamii ya wachimbaji madini ambaye anajua hasa kero na madhira ya sekta hii miaka nenda rudi, Dotto Biteko,Waziri wa madini pia historia haiwezi kumweka pembeni katika hili!

Bunge la Mh Spika Job Ndugai pia sura yake nzuri inabebwa na utekelezaji wa mapinduzi haya makubwa katika sekta ya Madini Nchini!”Mineral Revolution in Tanzania”Utungaji wa Sheria kuu tatu zilizopitishwa pale Bungeni jijini dodoma na wabunge asilimia karibia kubwa wakiwa wa chama dola yaani CCM mwaka 2017.

Risasi tatu ambazo ziliweza kuteka uwanja wa medani kwa maana ya sekta ya madini ni Sheria ya “The Natural Wealth & Resources Contract(Review & Renegotiations of unconscionable Terms)Act,2017.

Sheria ya pili ni ya “The Natural Wealth & Resource(Parmanent Sovereignty)Act,2017.Sheria hii inalipa bunge nguvu za kupitisha mikataba yote ya madini ambayo Nchi ya Tanzania itapaswa kuingia.

Sheria ya tatu ambayo imeweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya madini tangu uhuru ni Sheria ya “The Written Laws(Misceleneous Amendments)Act,2017!Sheria hii moja kwa moja imeleta mapinduzi makubwa katika sekta husika ambayo hayajawahi kuonekana kokote barani Afrika tangia uhuru,achana na Tanzania tu.

Sheria hii ndio imeweza kuipa serikali ya CCM uwezo wa kuwa na hisa katika makampuni ya madini kama mwekezaji mwenza kitu ambacho hakikiwahi kutokea tangia uhuru wa Nchi hii yaani tangia mwaka 1960.

Kupitia Sheria hizi,Serikali ya CCM imeweza kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya madini kuliko Nchi yoyote katika Afrika hii!Baadhi ya mapinduzi hayo ni!

HAYA HAPA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA MADINI TANZANIA TANGIA UHURU!

1.Historia ya sekta ya madini tanzania itawakumbuka hayati John Pombe Magufuli,Rais wa sasa,Mh.Samia Suluhu Hassan na waziri wa madini Mh. Dotto Mashaka Biteko kwa niaba ya Watanzania wote kwa kuweza kuunda Kampuni za kizalendo ya Twiga Mineral Corporation ndani ya makubaliano na kampuni kongwe ya madini duniani yaani Barrick ambapo Tanzania itakuwa na hisa ndani ya uwekezaji wa Barrick “shareholding”.

Katika muendelezo huo,kampuni nyingine ya kizalendo ya Tembo imeundwa na serikali kati yake na kampuni ya Kabanga Nikel na serikali ya Tanzania katika kutekeleza sheria namba tatu ya “Written Laws(Misceleneous Amendments),Act,2017.

2.Kwa mara ya kwanza tangia uhuru wa Nchi hii ,Tanzania iliweza kuvuna kiasi cha kodi ya Tsh 479+ Bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2020 chini ya Wizara ya madini!

Mapinduzi haya yanatokana na juhudi kubwa na uchapakazi wa viwango vya juu kabisa vya Serikali ya CCM hasa katika miaka mitano ya utekelezaji wa ilani yake ya mwaka 2015/2020.

3.Hatua kubwa nyingine ni ujenzi wa masoko ya madini kila kona ya Nchi hii!Nenda Chunya,nenda Geita,Nenda mwanza,nenda morogoro,nenda Arusha,nenda kokote unakoweza kutaja!

Masoko haya yamepunguza utapeli,uporaji wa madini na kuweza kuipatia Serikali ya CCM takwimu sahihi za madini yake!Zaidi masoko haya yameleta ajira kwa watanzania wengi,upatikanaji wa kodi ya serikali pamoja na kuongeza utajiri kwa wachimbaji wadogo wadogo Nchini!

4.Pamoja na mambo mengine,Tanzania ndio Nchi ambayo inasifika kwa sasa barani afrika kwa kuwa na mifumo bora ya uthibiti utoroshaji wa madini kwenda nje ya Nchi!Uundwaji wa vikosi kazi mbalimbali katika sekta husika imeleta kuongezeka kwa kasi ya ukamataji watorosha madini na kupunguza kwa kasi ya utoroshaji madini nje ya Nchi!

Kwa sasa mtu lazima mara mbili mbili kama anataka kutorosha madini ya Nchi hii kwani vyombo vipo macho usiku na mchana kuzuia kupotea kwa rasilimali madini ya Nchi hii!

Ni wazi kuwa wizara ya madini chini ya Mh. Waziri, Dotto Biteko inaweza kuwa ndio mhimili mkuu katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 kuifanya wizara hii kuchangia angalau asilimia 10 ya pato la Taifa na kwa spindi hii ya Serikali ya awamu ya sita,tutarajie kufikia lengo kabla ya wakati yaani mchango wa sekta ya madini kufikia asilimia 10 ya pato la Taifa kabla ya 2025.

Mwandishi ni kijana wa kitanzania,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,vyuo vikuu vya Saut na Tumaini Iringa na Mtia nia wa CCM,Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %