George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 4,2021.
Wakati Taifa langu la Tanzania likiwa katika kuziendea siku za kutimiza miaka sitini ya kupata uhuru tangia mwaka 1961 hapo desemba 9,2021, Watanzania zaidi ya milioni sitini walikuwa wanamngoja kwa hamu kubwa kumsikia na kumwona Rais wao Samia Suluhu Hassan huyu wa leo kwa kuamua kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa!
Uamuzi wake wa leo wa kuivunja Bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya Bandari na Bodi ya wakurugenzi ya wakala wa Meli Tanzania ni zaidi ya umakini na uwajibikaji wa Serikali ya awamu ya sita anayoiongoza!
Hayati John Pombe Magufuli aliwahi kusema nanukuu”….tumechezewa sana,…Mimi nimekaa serikali miaka mingi,…madudu yote nayajua….”.
Utofauti wa hayati RAIS John Magufuli na Marais wengine waliopita katika Taifa hili ilikuwa upo katika mambo makuu matatu;(i) uwezo wa taasisi ya Urais kutafuta taarifa za jinsi mambo ya serikalini yanavyokwenda kwa mtindo wa “Triangle” dhidi ya “single chain information source”.
Hayati John Pombe Magufuli hakuwa na maajabu makubwa sana katika utendaji wake wa kazi bali alikuwa na uwezo mkubwa wa kutafuta taarifa kwa mtindo wa mafiga matatu”Triangle sourcing of information”hivyo kuweza kujua uwozo mkubwa iliokuwa unaendelea katika taasisi za Umma!
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh na Mama Samia Suluhu Hassan hapaswi hata siku moja kuamini taarifa za watendaji wake moja kwa moja”chain information sourcing” kwani kufanya hivyo ni kufanya makosa makubwa!Sisemi vyombo vyake hasivitumie lahasha!Nasema lazima awe na vyanzo vya taarifa nje ya mifumo rasmi!
Uchawi mwingine ambao ulimfanya hayati John Pombe Magufuli aogopwe na watendaji wake hasa katika suala la kupambana na ufisadi na rushwa katika utumishi wa Umma, ilikuwa ni kuitumia style ya(Ii) “Naming & Blaming”.RAIS kwanza anapaswa kuwataja au kutaja mambo yanayoendelea serikalini lakini pili lazima pia akemee kwa sauti yenye ukali zaidi kama alivyofanya leo RAIS wangu Mh. Samia Suluhu Hassan,namnukuu.
“….. watu wanafanya mambo yao serikali alafu wanasema ufisadi umerudi awamu ya sita……sitokubali,sitokubali……”.
Hakuna kitu ambacho kinawapa Watanzania masikini raha na faraja kama kuona wana mlinzi mzuri wa maslahi ya Taifa(RAIS)”State Castodian”hicho tu kwao ni faraja tosha na kura zetu mwaka 2025 tunaweza kuzipata kupitia hapo.
Uchawi mwingine wa hayati Magufuli ilikuwa katika kitu kinaitwa(iii) “after naming & blaming them”,then “confront them” Hii ina maana kuwa RAIS lazima uwe na uwezo wa kuwavaa kwa hasira wafuasi wako au wateule wako wanaotaka kukukwamisha katika safari yako!
Huyu ndio Samia Suluhu Hassan ambaye nilikuwa namngoja tokea “akiwashe” kwa mara ya kwanza kwa kumtumbua Mfano, namba moja wa Bandari kipindi hicho,Mkurugenzi Mkuu Kakonko!
Kama Mh RAIS Samia Suluhu Hassan anaitaka kweli “iyena iyenaa” mwaka 2025 basi lazima twende kwa mtindo huu hapo juu!Hatuna namna kwa sasa!
Hili kazi iendeleee lazima tuache kuchekeana na Mh RAIS hapaswi kumwamini mtu tena lazima iwe ni mwendo wa “tight marking,bampa to bampa au kolikoli” na hapo lazima kazi itaendelea!
Mwandishi ni Kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa mwanafunzi wa zamani,”Cadet”,Chuo Cha maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi zamani,Chuo Kikuu Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+225784159968.