0 0
Read Time:4 Minute, 40 Second

“Hoja dhaifu za Chadema zajibiwa na kada kijana wa CCM”

Mchungaji Msigwa

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
December 11,2021.

Jana nimemsikiliza kada wa Chadema Mh.Mchungaji Peter Msigwa nikacheka tu,baadae nikapata nafasi nikamsikiliza Mbunge wa zamani wa Chadema Jimbo la Tarime vijinini Mh Ndugu yangu John Heche nikacheka zaidi ya mara ya mara ya kwanza!

Watu hawa wazito kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo yaani Chadema walionekana au wanaonekana walijipanga kuja kuishambulia Serikali ya CCM wakati huu ilikuwa inasherekea miaka sitini ya uhuru wa Nchi hii lakini pamoja na kujipanga kote bado walionekana kuwa na hoja dhaifu za kudandia dandia ambazo hazitoshi kuthibitisha kuhusu kauli zao kuwa tangia uhuru hakuna kitu cha maana kilichoweza kufanyika katika Tanzania!

Katika kuupa uhai mpango wao huo kupitia vyombo vya Habari- mbalimbali Nchini,kwamba hakuna kilichoweza fanyika katika Nchi hii ndani ya miaka sitini ya uhuru wetu na wakaja na hoja zifuatazo;

1.Makada hawa wazoefu ndani ya Chadema, wanasema mpaka tunafikia miaka ya 1960,Tanzania na Nchi ya Singapore zilikuwa sawa katika nyanja ya kiuchumi lakini mpaka leo Nchi ya Singapore wana uchumi wenye GDP zaidi ya USD 300+ Billioni wakati Tanzania mpaka mwaka 2020 ilikuwa na GDP ya USD 60+ Billioni.

Kwahiyo wanahitimisha kuwa Serikali ya CCM haina uwezo wa kuongoza Nchi hii mpaka sasa kutokana na tofauti hiyo ya pato la Taifa.

2.Hoja yao ya pili wanasema, miaka sitini ya uhuru wetu kama Taifa, mpaka leo, watanzania hawana huduma ya maji na umeme wa uhakika!

3.Lakini mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa zamani wa Iringa mjini anasema, katika kupima maendeleo yetu hatuwezi kujipima dhidi ya sisi wenyewe kama Nchi lazima tujipime dhidi ya wengine ili kujua kama tumeendelea au hapana!Hoja zao ukizisikiliza haraka haraka unaweza kudhani kuwa zinabeba mantinki kumbe wapi!

Labda nianze kujibu hoja hizi kitakwimu na uhalisia kuhusu dhana nzima ya maendeleo ya Nchi hii ya Tanzania dhidi ya Nchi za Tiger!

KWANINI TANZANIA MPAKA SASA HAIWEZI KUWA SAWA NA NCHI ZA TIGER?

Pamoja na ukweli kuwa mpaka miaka ya 1960 Tanzania na Nchi za Tiger kama vile Nchi za Singapore,Taiwan,Hong Kong na South Korea zilikuwa sawa kimaendeleo lakini kuna sababu za msingi zilizoifanya Tanzania isikimbizane na Nchi za Tiger mpaka sasa na sababu ni hizi HAPA;

1.CDM wanapaswa kujua historia kabla ya kudandia hoja kwani hakuna Nchi yoyote kati ya Nchi ya Tiger ambayo tangu mwaka 1960 mpaka leo imewahi kuingia katika vita wakati Nchi ya Tanzania mwaka 1978, iliingia kwenye vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda na kuweza kuharibu uchumi wote wa Tanzania!

Baada ya vita vile Nchi ya Tanzania ni kama vile ilikuwa inaanza kujenga upya uchumi wake na kuanza kifikilia kuchukua mkopo wa haraka wa 150 millioni USD kuweza kurudisha uchumi ulikufa kabisa KABISA!Wakati haya yanatokea labda Kijana kama John Heche alikuwa hajazaliwa, hawezi kuyajua haya!

2.Tangia miaka ya 1960, hakuna angalau Nchi hata moja ya Tiger kama vile Taiwan ambayo iliwahi kukumbwa na ukame wa kutisha wakati huo Nchi ya Tanzania kati ya miaka ya 1974/75 ilikumbwa na ukame ambao haujawahi kutokea hivyo kufanya kushuka kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa viwandani!

3.Wakati miaka ya 1960 idadi ya watu mfano, katika moja ya Nchi ya Tiger, ilikuwa watu 2.11 millioni tu wakati idadi ya watanzania kwa mwaka huo huo ilikuwa angalau 14 millioni!Mwaka 2020,idadi ya watu Nchini Singapore ilikuwa watu 5.69 millioni tu huku idadi ya watanzania ikifikia watu 59.7 millioni karibia mara kumi ya watu wa Singapore!

Nataka kusema nini?ni rahisi kwa Nchi ya Zanzibar kupata maendeleo ya haraka kuliko Tanzania bara kutokana na ukubwa na Nchi na kigezo cha idadi ya watu!Serikali inakuwa na mzigo mkubwa zaidi wa kutoa huduma kwa watu hasa pale panapokuwa na idadi kubwa ya watu na ukubwa wa eneo la mraba!

HOJA YA UKOSEFU WA HUDUMA ZA JAMII ZA KUTOSHA.

Ni wazi kuwa ubora wa huduma yoyote ambayo Serikali inaitoa utegemeana sana na idadi ya watu katika eneo husika!Umewahi kufikiria kwanini shule bora katika matokeo ya mitihani yao ya kitaifa utegemea sana idadi ya wanafunzi waliopo darasani?!

Ni rahisi mno kwa Nchi ya Singapore kuwafikishia huduma za jamii watu 5.69 millioni katika eneo dogo na hivyo hivyo, inakuwa ngumu mno kwa Nchi kama Tanzania yenye watu zaidi ya 59.7 millioni kwenye eneo la km za mraba la zaidi ya sq meter zaidi ya 300,000 kuwafikishia huduma hiyo hiyo ndani ya miaka sitini tu.

2.Asilimia kubwa ya uchumi wa kwa Mfano Nchi ya Singapore hasa kwenye sekta ya huduma unabebwa sana na makampuni binafsi kupitia CSR Policy ambapo Nchi hiyo imeweza sana kujenga sekta binafsi iliyo shindani hivyo kuipunguzia Serikali shughuli za kutoa huduma kwa watu wake!

3.Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa Nchi chache zilizopo barani Afrika ambazo zimeweza kwa asilimia karibia 90% kutekeleza sera ya umeme vijijini”Rural Electrification”.Maeneo mengine ambapo Nchi ya Tanzania imefanya vizuri ni katika eneo la afya!

Ni wazi kuwa,Nchi ya Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa ndani ya miaka sitini japo juhudi zaidi na zaidi zinahitajika katika kuhakikisha spidi ya kuleta maendeleo inaongezeka zaidi ili kuweza kwenda sambamba na idadi ya watu wake wanakaribia kufikia millioni sitini, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2012.

Jicho la Uledi ni makala za uchambuzi wa siasa nchini na kimataifa zinazo andikwa na Mwandishi kijana msomi wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Saut & Tumaini Iringa na Mtia Nia wa ubunge Jimbo la Kyela CCM 2020.

contact:+255784159968.

WU®

©2021 WABONGO UGHAIBUNI

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %