0 0
Read Time:5 Minute, 26 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 29,2021.

Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kudai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia Trilioni 70, ”ipo siku nchi hiyo itapigwa mnada”.

Ndugai aliyasema haya katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma.

Spika ndugai alisema ni vyema Tanzania ijitegemee yenyewe kwa tozo na makato mengine kwa maendeleo na wala sio kukopa.

Juzi Mama (Samia Suluhu Hassan) amekwenda kukopa 1.3 trillion deni.Tuna majengo hivi sasa madarasa vituo vya afya ambayo yanajengwa kwa tozo. Ipi ni bora, sisi Tanzania ya miaka 60 tuendelee kukopa madeni makubwa makubwa yasioeleweka au tubanane tufanye wenyewe hapa?”

Hivi sasa deni letu ni 70 trilinioni” Is that healthy ? ”Madeni, Madeni, Madeni, Iko siku nchi hii itapigwa mnada”. Bajeti yetu ni Trilioni 30 na kumi katika hizo tunalipa madeni kila mwaka.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alisema “Tutakopa tumalize miradi ya maendeleo ili tuendelee. Ukikopa unajenga sasa tena kwa haraka, ukisubiri ukusanye mapato ya kwako utamaliza lini kujenga? Mradi wa Matrilioni unasubiri za kwako utaumaliza lini” Rais Samia amesema hayo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Makutupora kwenda Tabora.”

HOJA NZITO NDANI YA KICHWA CHEPESI CHA MH. SPIKA JOB NDUGAI.

Wajibu wa kibunge katika Nchi zote duniani ni kuishauri na kuisimamia Serikali kupitia platform ya chombo kinachoitwa Bunge na katika mazingira haya, tunazungumzia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Job Ndugai!

Mawazo ya Mh. Spika Job Ndugai bila kupepesa macho ni mawazo ya mtanzania yoyote ambaye anawaza nje ya box na pia anayeiwaza Tanzania ya kesho itakuwaje baada ya miaka mia moja mingine mbele!

Niliwahi kuandika kuwa “Tunataka kuwa Taifa kubwa wakati VIONGOZI wangu wanawaza mambo madogo madogo,haitowezekana”.Angalau kwa mara ya kwanza MH. Spika Ndugai anaongea mambo makubwa lakini kwa wepesi na ndio maana na sisi tumeweza kumjibu kiwepesi wepesi TU!”Je,Spika Ndugai Hapaswi Kuhojiwa na CCM?”.

Nimekuwa nikipiga kelele kila siku kwenye maandiko yangu kuwa hauwezi kuifungua Nchi na kuweza kupata maendeleo ya kweli kwa kutokea nje, hapa namaanisha kuwa hauwezi kutengeneza Tanzania imara,shindani na kutaka kuwa Taifa kubwa kwa mawazo ya mikopo kutoka nje,uwekezaji kutoka nje,kuamisha tekinolojia kutoka nje”dependency”.

Unaweza kutengeneza Taifa imara kiuchumi kwa kutokea ndani kwako na kwenda nje ya mipaka yako!Taifa lolote serious uanza kuitafuta nguvu yake ya ndani na kuitawanya nje ya mipaka yake baada ya watu wake wa ndani kushiba!

Bahati nzuri sana nguvu yetu ya ndani kama Taifa ni kubwa mno kuliko nguvu tunayoangaika kuitafuta nje ya mipaka yetu lakini nadhani tunakosa uongozi wenye ndoto kubwa,akili kubwa na leadership mobility TU!

Uchumi wa vijijini pekee yake ungeweza kutupa zaidi Trilioni 30 Tsh kwa mwaka kama tungekuwa na akili kubwa!Kilimo cha mawese pekee yake kwa mwaka 2017, kiliweza kuingizia Nchi ya Malaysia kiasi cha Dola za kimarekani Billioni 23 USD.

Tanzania imekuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kila mwaka kununua mafuta ya kula nje ya Nchi na labda kiasi hicho kingeweza kutumika ndani ya Nchi katika shughuli zingine za kujenga uchumi!Unashanga kwanini fedha za mikopo yetu haziendi katika maeneo ambayo yangeweza kujenga uwezo wetu wa ndani?”export muscles”.

Wakati Tunapiga kila mwaka kuhusu sukari,Nchi ya Brazil inajipatia mabilioni ya dola kwa kuuza sukari yake nje ya mipaka yake!Hauwezi kuifungua Nchi bila kuifungua sekta ya uchumi vijijini”Rural economy”.

Sekta ya vijijini ina uwezo wa kutupa Trilioni mpaka 30 kwa mwaka almost bajeti yetu ya mwaka!Sekta hii inabeba uchumi Kilimo,uchumi MADINI,Uchumi Ufugaji,Uchumi bidhaa za mbao!

Unabisha?Uchumi wa wilaya kama Chunya na Songwe Mkoani Mbeya na Songwe unabebwa na sekta ya MADINI dhahabu pekee yake!Uchumi wa wilaya Mufindi unabebwa sana na Uchumi Mbao,Uchumi wa Mkoa wa Arusha unabebwa pia na Kilimo cha maua.Utajiri wa watu wa maeneo niliyoyataja hapo juu ni matokeo ya shughuli hizo!

Swali kubwa hapa ni je,Serikali yangu ya CCM inashindwaje kuzitawanya “case studies” za maeneo haya katika maeneo mengine?Mh. Spika Job Ndugai katika hoja yake alipaswa kumwambia haya Mh. RAIS na Mwenyekiti wetu wa CCM na sio kumtishia kupitia uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 tuu!

Je,tunaye mtu anayewaza kuifungua Tanzania kutokea ndani?yupo WAPI?Kwa Kifupi kuifungua Nchi kwa kutokea nje,nasema hauwezi kukwepa mambo yafuatayo;

1.Utegemezi wa milele!uzoefu unaonyesha kuwa tangia tupate uhuru, Tanzania tumekuwa na miradi mingi ya maendeleo lakini mingi ilifia njiani kutokana na kukosa “continuity”.Ulitegemea miradi kama ya mabasi ya enzi zile ya KAMATA na UDA ndio ingekuwa leo inaendesha sekta ya usafiri nchini, lakini baada ya miaka 60 ya uhuru, Nchi inaongelea miradi ya UDART tena!Tunapiga hatua 10 mbele na kurudi hatua tisa nyuma!

Nataka kusema Nini?mikopo kutoka nje haijawahi na haitowahi kuisaidia Nchi hii kuweza “kumaintain continuity” ya maendeleo ya Taifa na ndio maana mpaka leo tumeendelea kukopa kwa ajili ya “kuservice” madarasa,vyoo na sekta afya!Hii ni aibu kwa Taifa kubwa kama Tanzania,haiwezekani!

2.Kuifungua Nchi kupitia uwekezaji toka Nje haitupi uhakika wa kitu kinaitwa “economic sustainability”!Uwekezaji toka nje uja na kuondoka na haukupi uhakika wa maendeleo ya muda mrefu!Je,kiwanda cha Urafiki kipo wapi Leo?!Hivi ndugu yetu Dangote akiamua kufunga kiwanda chake tunaweza kumzuia?!Biashara za kimataifa zina tabia za kuamaama kutafuta fursa katika maeneo mengine!Sasa unawezaje kuweka “moyo” wa Uchumi wa Taifa lako katika uchumi “fake” kama huo?tunapaswa kuwaza pamoja!

3.Tungekuwa tunawaza vizuri, kwanini mkopo wa UVIKO-19 wa Trilioni 1.3 tusingeupeleka kwenye kufanya Mapinduzi makubwa kwenye sekta yetu ya afya?HIVI hatuna ndoto ya kuwa na APOLO ya Muhimbili?Hivi hatuna ndoto ya kutengeneza chanjo zetu?Hivi hatuna ndoto ya kuendeleza mafanikio makubwa ambayo yameweza kuanzishwa na yule Major Generali wa pale MSD kwa kuanza kutengeneza Panadol zetu na vifaa tiba vyetu?

Ndio maana nasema,Mh.Spika Job Austino Ndugai anabeba maono makubwa lakini katika kichwa chepesi sana!Kumshambulia Mama Samia SULUHU HASSAN kwamba asichagulike Mwaka 2025, ilikuwa ni akili nyepesi MNO bali alipaswa “kumchallange” Mh.RAIS wangu na mwenyekiti wake wa CCM Taifa, angalau kwa “vihoja” vyangu HIVI!Mjadala ungekuwa very positive kuliko ulivyo hivi sasa!

SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH.JOB NDUNGAI

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa za zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Chuo Kikuu Cha Saut & Tumaini na mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %