0 0
Read Time:5 Minute, 49 Second

WU®

Mnamo Desemba, 2021,Bunge la Congress la Marekani liliweza kupiga kura kuhusu kama kuna umuhimu wa Taifa kubwa duniani la Marekani kuendelea kukopa au kutokuendelea kukopa!Vyama vikuu viwili Nchini humo vya Democrat na Republican vilikuwa vinavutana kuhusu ustahimilifu wa deni la Taifa na kuitimishwa na hoja kwamba, Serikali ya Marekani haipaswi kukopa tena kwa sasa!

Ukubwa au udogo wa hoja ya Mheshimiwa Spika Job Ndugai, kuhusu mikopo ambayo tumeendelea kuichukua kama Taifa leo, labda inaweza kuanzia hapo!

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU MH. SAMIA SULUHU HASSAN
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 29,2021.

Sio CDM tena chama kikuu cha upinzani cha wakati fulani Nchini Tanzania ndicho ambacho kwa sasa kinachoivuruga serikali ya awamu ya sita bali ni uwepo wa makundi ya wazi wazi yanayozidi kujijenga ndani ya CCM ya sasa.

Mpaka dakika hii, sijaona mapungufu makubwa ya wazi ya serikali ya awamu ya sita ya Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan, ukizingatia kwamba haijatimiza hata mwaka mmoja madarakani kiasi kwamba tunaweza kufanya evaluation na kutupa majibu ya kushindwa ama kufanikiwa kwake!

Wote tunajua nguvu za Bunge kwamba, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lina uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mh.Rais na Mh .Rais anaweza kuondoka”Impeachment”!Bunge letu lina nguvu hizo kama “conditions” fulani fulani zitakuwa zimetimia!

Lakini pia Bunge la Spika Job NDUGAI, lina uwezo wa kuikwamisha Bajeti kuu ya serikali na serikali ikashindwa kutekeleza malengo yake ya kitaifa ikiwemo lile lengo la kiilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/25.

Mpaka hapo, unaweza kuona “ukubwa” na “ukali” wa maneno na kauli za Mh. Spika Job NDUGAI,nanukuuu;

“….tusubili tuone mwaka 2025 tuonae kama mtachagulika,…wakiamua kuchagua wengine SAWA,wakiamua kuwarudisha ninyi ili mkaendelee kukopa sawaaa….kuna siku NCHI itapigwa mnada hii…..”.

Kama sikosei Spika Job NDUGAI ni sehemu ya vikao vya juu vya CCM,ana nafasi kubwa ya kutoa ushauri wake ndani ya chama na serikali!Kwa kauli rahisi, maneno haya ya Mh.Spika Job NDUGAI yanapaswa kumwandaa Mh. Rais Samia SULUHU HASSAN kwa lolote!Hii ni vita KABISA KABISA!

Always wanaoshinda vita katika uwanja wa medani sio tu kwamba ni wale wenye silaha bora bali pia inaweza kuwa ni wale wenye mbinu bora za medani “Maneuver”.

Kauli ya Spika Job NDUGAI sio kauli rahisi sana na Mh.Rais Samia SULUHU HASSAN anapaswa kuandaa “mpango vita mapema” kwani kudharau au kuchelewa kuandaa mpango huo kunaweza kuleta hasara KUBWA NDANI ya ngome yake!”undermining the enemy is half defeat”!

KWANINI HAYA YANATOKEA SASA?

Katika makala zangu za huko nyuma niliwahi kusema na kuonya kuwa”kitendo chochote cha “kumnawa” JPM kinaweza kuwa na madhara makubwa ndani ya chama chetu CCM”.Sitaki kuamini kuwa haya yanayoendelea ni matokeo ya makosa makubwa ya kistrategia ambayo tumeyafanya ndani ya chama tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli!

1.Kitendo cha serikali ya awamu ya sita kutaka kujitenga na serikali ya awamu ya tano, wakati serikali yenyewe ya awamu ya sita imepata uhalali kutokana na awamu ya tano kwa maana ya kuendelea kutumikia Ilani ya awamu ya tano ni makosa makubwa kisiasa!

“….haya yanayotokea yalianzia huko nyuma lakini watu wanataka kuiangushia mzigo awamu ya sita,….sitokubali….”.

“….tulitumia nguvu kubwa na kuanza kuonea watu,….kodi ya dhuluma hapana….”!

2.Kushindwa kwetu kukalipia kundi ambalo lilionekana wazi wazi kijipanga kimkakati kutaka Kumshambulia JPM huku viongozi wangu wa juu wa CCM wakiwa kimya ilionekana kuwa labda, mpango ule ulikuwa na baraka za safu ya juu ya chama!Katika hili hakuna mtanzania ambaye ametuelewa hasa katika ukimya wetu!

3.Kushindwa kwa mhimili wa serikali kuliheshimu Bunge ndiko kumemwibua Spika Job Ndugai mpaka akatamka maneno mazito kiasi kile!Niweke wazi kuwa vyovyote iwavyo,Spika Job Ndugai hakupaswa kutamka yale maneno hadharani!

“…ngoja 2025 tuone kama mtachagulika….wakichagua wengine SAWA,wakichagua hawa hawa sawa..ili wakaendelee kukopa…..kuna siku NCHI itapigwa mnada,…haiwezekani tukaendesha NCHI Kwa namna hii…..”.

Ndugai anasema”…tulipitisha tozo kibabe tukasema utake usitake tutatoza….”.

Ni kama Spika Job Ndugai anasema Serikali imelisaliti Bunge wakati Bunge liliwahi kuwa “PUNDA” wa Serikali, kwa kupitisha tozo za miamala ya simu japo watanzania WENGI waliikataa!Hapa pana hoja nzito KIDOGO kwani Serikali na Bunge vinapaswa kulindana”cover”.

Kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuamua kutofautiana na wananchi kwa lengo la kuibeba Serikali ya awamu ya sita ili kuweza kupata mapato ambapo Bunge kupitia Mh. Spika Job Ndugai waliweza kusimama kidete na kupigia debe kuwa, tozo zile zingeweza kuleta barabara vijinini,ujenzi wa madarasa na hospitali na huduma zingine za jamii kimejibiwa tofauti na Serikali!

Miezi mitano tu baada ya kuanza kutoza tozo kwenye miamala ya simu, Serikali ikaugeukia mkopo kutoka IFM, wa Tsh Trilioni 1.3 kwa ajili ya “same same mission” yaani katika ujenzi wa madarasa!

Ni wazi kuwa tafsiri rahisi hapa ya Mh.Spika Job Ndugai ni kwamba, Serikali ni kama linalidharau Bunge na ndio hapo Mh. Spika Job Ndugai anataka na yeye kutunisha msuli wake na kuitafuta heshima ya Bunge!Vita yote hii inaanzia hapa na sio sehemu nyingine!

CCM TUNATOKAJE HAPA TULIPO KWA SASA?

1.Hasira zile za Ndugu Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanzania “zinaback up” kubwa na hazipaswi kuchukuliwa powa!

Spika Job Ndugai anaweza kuwa chambo tu cha watanzania wengi ambao hawataki kuona dhihaka dhidi ya Serikali ya awamu ya tano zinaendelea huku, viongozi wa awamu ya sita wakishindwa kukemea!Ukitaka kujua ilo basi jiulize kwani Rais Samia Hassan kakopa Tsh. ngapi mpaka sasa?,kwani Spika Job Ndugai hakuwepo wakati zinakopwa za awamu ya tano?!Hapa issue sio mkopo,kuna kitu kinatafutwa either kizuri au kibaya!

2.Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM ,anapaswa kuliacha hili lipite,kwangu mimi naona, nguvu yoyote ya kibabe ya kumsurutisha Spika Job Ndugai inaweza kuleta madhara makubwa kwa CCM na Serikali yake kwa sasa!Silence is not ignorance”

Kama CCM tuna “political strategist” wazuri, wanapaswa kuingia kazini sasa na kuanza kuunga mkono hoja ya Mh. Spika Job Ndugai Ili upepo huu upite, kinyume cha hapo tutajikuta tunaingia katika mgogoro mkubwa kati ya Bunge na Serikali!

Natamani atoke “kingunge” mmoja ndani ya CCM na kukubali kuwa hoja ya Spika kuhusu mikopo tunaenda kufanyia kazi ili kuweza kuzima mjadala huu kimkakati!Bahati Mbaya sana, Mh Rais ameshasema tutaendelea kukopa!

3.CCM kamwe isije kuruhu ule upande wa pili “wale wa kuleeeeeee” waje wajibu hoja hii tena kwa lengo la kutaka kujikomba kwa Mama kwani ndio moto utakuwa unawaka upya tena!

Hapa naongelea kale kakundi kalikosema “JPM achunguzwe kwa kukopa sana”!Kuruhusu kale kakundi ni kuwasha moto upya tena hivyo kudhofisha uhai wa CCM yangu!CCM inahitaji Utulivu sana kwa sasa maana hii vita sio tena kama ile ya Gwajima,Slaa na PolePole,hii ni nzito sana!

Bwawa la Nyerere #Kaziinaendelea

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut & Tumaini Iringa,Mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

HAPPY NEW YEAR WATANZANIA NA WAZALENDO WOTE!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %