George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 31,2021.
Idara ya yetu ya Habari-Maelezo kimsingi ndio ilitakiwa kuwa chombo maalum cha serikali ama kwa kingereza “planner & changers” kwa kuweza “kucontrol flow of information,news & events” ndani ya Nchi hii ili kuifanya Serikali iweze kufanya kazi zake bila kuwa na stress toka mitandaoni,magazetini,Radioni”mainstream media” na hata kwenye folk media!
Idara yetu ya Habari -Maelezo inatambulishwa kama ndio Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!Katika dhama hizi za kuenea na uwepo wa kasi kubwa ya kuenea kwa habari, zingine habari zenye nia mbaya,idara ya Habari-Maelezo ilipaswa kuwa ndio “information game changer” ili kuifanya Serikali iweze kufanya kazi zake bila stress!
WHY NAISHANGAA IDARA YANGU YA HABARI-MAELEZO?
1.Mpaka dakika hii,idara yangu ya Habari-Maelezo imekuwa kimya kuhusu upotoshaji unaoendelea kwenye mitandao ya jamii hivyo serikali kuonekana haifanyi kitu chochote au haijafanya chochote.
Kwa mfano,hivi idara YANGU ya Habari imeshindwa kujustify kwa nini MH RAIS alienda kukopa fedha za IFM na kuzipeleka kwenye ujenzi wa madarasa japo kulikuwa na fedha za tozo kwenye miamala ya simu?
2.Idara yangu ya habari-Maelezo hivi inashindwa kujustify kuwa serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani ilikuta “mafaili” kibao mezani ya madai ya watumishi wa umma ambao hawakuwahi kupandishwa mishahara,kupandishwa vyeo na hata madaraja kwa zaidi ya miaka mitano kinyume na sheria za utumishi wa umma!
3.Katika mwaka wa fedha wa 2021/22,askari Polisi zaidi ya 2000 walipandishwa vyeo kutoka kuwa askari wa kawaida(NCO’s)mpaka kuwa maofisa wakaguzi wa Polisi!(Sub Inspectors).
4.Zaidi ya askari 4000 wa vyeo vya chini yaani (NCO’s) wamepandishwa vyeo Katika ngazi mbalimbali,zote hizo hela na sio vijisenti viwili au vitatu!
Kaka George Simbachawene anaweza akatupa takwimu za kihesabu na fedha kiasi ambacho Serikali imetumia katika shughuli hizi!
5.Zaidi ya ajira 1500 mpaka sasa zimetolewa Nchini katika vyombo vya Polisi,Magereza,Uhamiaji,Takukuru,Zimamoto ndani ya mwaka mmoja tu wa serikali ya awamu ya sita!Hizi zote ni Mabilioni ya fedha zikiwemo za tozo za miamala ya simu!
Ajira mpya,kupandishwa madaraja watumishi wa umma kunaweza kukawa kumetumia fedha nyingi zaidi ya tulizokusanya kwenye tozo za miamala ya simu!
MENGINEYO AMBAYO IDARA YA HABARI -MAELEZO INAPASWA KUJUSTIFY!
1.Serikali inatarajia kulipa zaidi ya Trilioni 2+ kwenda kwenye mfuko wa PSSSF kusettle madeni ya muda mrefu ambayo awamu ya sita imeyakuta mezani!
2.Ndani ya mwaka mmoja,Rais Samia aliweza kutoa shilingi Milioni 500 kwa kila jimbo zaidi ya majimbo 200+ Tanzania nzima, kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu katika majimbo hayo!
3.Bajeti ya Bodi ya mikopo ya elimu ya juu iliongezeka na idadi ya wanufaika iliongezeka pia kwa maana ya wanufaika wa mikopo kwa zaidi ya Bilioni kadhaa!sina takwimu hapa!
4.Kumbuka kuwa hii ndio Bajeti yake ya kwanza MH Rais Samia Hassan lakini ameonekana kutibu mambo mengi na sasa watumishi wa umma wameanza kutabasamu!
Kijana wangu mmoja mtaani jana kanipigia simu anasema”….baada ya miaka kadhaa ya kukaa mtaani tangu nimalize elimu YANGU mwaka 2016,,angalau kwa mara ya kwanza nimeitwa kwenye interview ya PCCCB
….”.amefurahi kweli!
Wana idara ya Habari -Maelezo tubadilike KIDOGO!Ndani ya mjadala mkubwa wa tozo vs mikopo tumewachia Watu wa kawaida kuitawala mijadala wakati sisi tupo na tunajua nini tunapaswa kufanya then why we are not doing?
Tukishindwa sisi kumsemea Rais na Serikali yake ambao kimsingi ndio wajibu wetu namba moja, wengine watauchukua wajibu huo na watasema wanalojua wao!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut na Tumaini Iringa na Mtia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.