0 0
Read Time:3 Minute, 12 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
February 8,2022.

Mama Samia Suluhu Hassan uwenda akawa Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kura nyingi zaidi!

“…wanashangaaa kuona yule waliyempa daraja fulani ndie anafanya haya …” Samia aliwahi kunukuliwa ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuimudu kazi husika na utayari wake kuelekea mwaka wa uchaguzi wa 2025.

Mpaka sasa rekodi nzuri zaidi ya Rais mwanamke kupata ushindi mkubwa zaidi,inashikiliwa na Mwanamama aliyekuwa Rais wa Liberia wakati fulani Ellen Jahnson Sirleaf ambaye angalau alishinda kwa asilimia 50+.

Habari nyema kwa Chama cha Mapinduzi yaani CCM na wafuasi wake ni kwamba Mh. Rais Samia Suluhu hassan ameendelea kuonyesha kuimarika na ukomavu wa viwango vya juu kabisa kiasi kwamba wale wote waliodhani labda 2025 ndani au nje ya Chama itakuwa kazi rahisi kwao wameanza kukata tamaa!

Mambo makubwa matano ambayo ni dhahiri yameweza kubadilisha mitazamo ya watu wengi kuhusu umakini na uimara wa Rais Samia Suluhu hassan katika nafasi yake ya urais ni haya hapa na uwenda kazi ikawa rahisi sana kwake 2025.

1.Kuendeleza ajenda ya miradi ya kimkakati kwa spindi Ile Ile ya awamu ya tano!Wengi walidhani kuwa mabadiliko ya
uongozi ndani ya chama na serikali yangeweza kuifanya baadhi ya miradi kuathirika lakini wapi!

“….Mimi na JPM ni kitu kimoja…” Samia aliwahi kusema na hii inathibitishwa na uendelezwaji wa reli ya kisasa ya standard gauge kuelekea nchi za Rwanda na Jiji la Mwanza!

2.Usimamizi bora wa rasilimali za Taifa hasa sekta ya madini!Mh Rais ameendelea na usimamizi makini katika sekta ya madini kupitia waziri wake makini PhD Dotto Biteko ambaye kwa kiasi kikubwa ameonyesha ufanisi na mafanikio makubwa katika sekta husika!

“…huyu kaka yangu Kabudi nataka nimtumie katika mikataba yote ambayo Nchi itaingia…amefanya kazi nzuri sana kwa Taifa…” Rais Samia aliwahi kunukuliwa!

3.Ukali kwenye fedha za Umma!Rais ameonyesha wazi kuchukuzwa na “upigaji” ndani ya Serikali yake!Rejea sakata la wafanyakazi wa Bandari ambao wapo na kesi za kujibu mahakamani!

Rejea kutumbuliwa kwa wakurugenzi wanne wa majiji na Halmashauri za Mbeya,Singida,Iringa na kwingineko!

“….nilisema mkitaka kujua rangi yangu nendeni kacheeni hizi fedha,…kuanzia Sasa nimetengua wakurugenzi wa Iringa,Mbeya,Singida ….”.Rais Samia alisikika wakati wa ziara yake kuelekea jijini Mwanza!

Hii ni ishara ya kuwepo kwa commitment na umakini wa viwango vya juu kabisa katika kusimamia fedha za Umma!

4.Kuendeleza sera za ukombozi wa mwanamke NCHINI!Ni wazi kuwa Serikali ya awamu ya sita imeacha Alama kubwa isiyoweza kufutika katika harakati za usawa wa jinsia katika siasa na uongozi wa Tanzania mpaka sasa!

“…niliamua kuvunja Ile tabia kwamba pale Wizara ya ulinzi lazima akae Mwanaume…..”Rais aliwahi kunukuliwa akisema baada ya uteuzi wa Mh Tax.

Uwepo wa Spika wa Bunge Mwana Mama na Mawaziri wengi wakinaMama ndani ya Baraza la mawaziri kunamfanya Rais Samia kuwa Rais wa kwanza barani Afrika kuwahi kufanya teuzi nyingi za kina Mama na wanawake katika nafasi nyeti za Serikali na kisiasa ndani ya kipindi Kifupi!Nini mnataka!

5.Sifa nyingine ambayo unampa Samia upekee ni uwezo wake wa kutotabilika kwa wafuasi wateule wake!

Pale unapodhani Mh Rais Samia Suluhu hassan hana taarifa zozote kuhusu jambo fulani ndio wakati ambao anaweza kukuumbua hadharani na pale unapodhani atafoka basi ukaa kimya!

“…nilikuwa nikufyatue RC Mara..bora umesema mwenyewe…”amenukuliwa akisema alipokuwa Mkoani Mara.

“….yaani polisi mnashutumiwa kufanya mauaji alafu mnataka kujichunguza wenyewe…..Nakuagizia Waziri Mkuu,kuunda tume haraka,alafu tuje tufananishe repoti ya Polisi na repoti ya Tume alafu tuchukue hatua….”.

Ni wazi kuwa kukubalika kwa Mh Rais kunaongezeka siku hadi siku hivyo kuifanya kazi ya CCM mwaka 2025 kuwa rahisi kuliko kumsukuma mlevi!

Mwandishi ni Ofisa za zamani Idara ya habari-Maelezo,Ofisa wa zamani Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mkufunzi wa zamani Chuo Kikuu cha Tumaini na Saut- Tabora na Mtia wa ubunge wa CCM Jimbo la Kyela mwaka 2020.

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %