
WU®
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
February 9,2022.
Maneno ya RAIS wangu Mh.Samia Suluhu Hassan leo Jijini Dodoma wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara mzunguko, kwamba bado Mh Samia anaisikia sauti ya mtangulizi wake , hayati John Pombe Joseph Magufuli ni zaidi ya kuiteka ngome ya adui huku ikiwa na silaha zote za kivita!
Kwa maoni yangu ni kwamba CCM tayari inabeba mtaji wa kura zaidi ya 80% za watanzania kwa kujifungamanisha pekee yake na hayati John Pombe Magufuli!Labda ubishi na “umwamba” wetu ndio unaweza kutuponza kwani “survey” ya haraka haraka ya kitaani kwetu, hapana shaka kuwa, CCM mpaka sasa, inaweza kuwa na mtaji wa kura wa asilimia mpaka 80% za kuweza kushinda uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Tunahitaji kukiri tu kuwa tupo hapa kutembea katika ndoto za Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/25 na zilizokuwa ndoto za hayati John Pombe joseph Magufuli na Makamu wake wa RAIS wakati huo Mh. Samia Suluhu Hassan kwani kwa kufanya hivyo 2025 yetu inaweza kuwa rahisi sana!
Watanzania wanatakiwa wajue kuwa Serikali ya awamu ya SITA ni muendelezo wa kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kilichobadilika ni “dereva” tu KWANI gari letu bado ni lile lile yaani CCM.
“…nasikia sauti ya hayati John Pombe Magufuli kuhusu miradi hii ya kimkakati….”RAIS wangu Samia Suluhu Hassan amenukuliwa leo jijini Dodoma!
Kutembea kwenye kauli kama hizi zinazo enzi kazi kubwa na nzuri za hayati John Magufuli na Makamu wake wa RAIS wa wakati huo Mh. Samia Suluhu Hassan, inaweza ikawa “strategy nzuri” ya kusaka maendeleo yetu kama Taifa na kusaka USHINDI wetu mkubwa tunaungojea kama wanaccm kuelekea mwaka 2025.
Tukifanya makosa leo ya kuikataa “political maleage” hii ya bule bule aliyotuachia hayati John Pombe Joseph Magufuli, wenzetu wapinzani wataitumia vizuri zaidi kutubomoa kuelekea mwaka 2025.Kwanini tukiogope kukisifu kinyago chetu tulichokichonga wenyewe?
Kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama chetu yaani CCM, tunapaswa kumuunga mkono Mh. Mama Samia katika kuimba wimbo mmoja kwamba;
“….Mimi na hayati Magufuli ni kitu kimoja,….nasikia sauti ya hayati Magufuli,….Siwezi kuvaa viatu vya hayati Magufuli,…”.
Tukishaelewana kuwa CCM yetu ni moja,Ilani anayoitumia Samia Suluhu Hassan ndio Ile Ile aliyoitumikia hayati John Pombe Magufuli!
Ndio maana tulianza na HAPA KAZI TU na baada ya msiba ule mzito wa kitaifa wa kuondokewa na Kamanda wetu,Sasa tunasemaa ACHA KAZI IENDELEEE chini ya JEMEDARI mwingine,Mh Samia Suluhu Hassan!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa mwanafunzi wa zamani Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mdhahiri wa zamani vyuo vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na mtia nia Ubunge Jimbo la kyela 2020.
+255746726484.