0 0
Read Time:2 Minute, 14 Second

Tumemuona Ndugu yetu (Prof Jay) hali yake inazidi kuimarika, tumshukuru Mungu lakini niwashukuru madaktari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kumhudumia, pamoja na mchango huu wa kuwezesha matatibu lakini kwa Niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Mhe.Rais Ndugu.Samia Suluhu Hassan niwahakikishie tutaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha matibabu yanaendelea vyema huku tukiendelea kumuombea apone haraka” Alisema Katibu Mkuu Ndg. Daniel Chongolo.”

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
February 10,2022.

WU®

Msingi mkuu wa kuanzishwa kwa Chama cha mapinduzi kikizaliwa kutokana na muungano wa vyama viwili vya Afro-Shiraz na Tanu mwaka 1977 unabaki katika dhamira ya kweli ya kujenga Taifa la Tanzania lenye watu wenye umoja na mshikamano.

CCM imeendelea kuwa Chama chenye kuamini katika falsafa ya undugu wetu ndio umoja wetu tangia kuanzishwa kwake na hata wakati wa uwepo wa TANU huko nyuma!

Katika ahadi kumi za MwanaTANU,ahadi ya kwanza na ahadi ya saba zinasomeka hivi,Nanukuu;

“…Binadamu wote ni ndugu na Afrika ni moja…”.Ahadi ya kwanza!

“….nitashirikiana na wenzangu wote kujenga Nchi yetu…”.Ahadi ya saba inasomeka!

Chama cha mapinduzi kinabaki kuwa Chama pekee cha mfano barani Afrika katika kusimamia misingi na falsafa za kuanzishwa kwake zaidi ya miaka arobaini iliyopita hasa wakati huu kikisherekea miaka 45 tangu kuanzishwa kwake!

Katika kuthibitisha hilo,Leo Katibu Mkuu wa CCM Taifa Komredi Daniel Chongolo akiongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa,Komredi Shaka Shaka, wamemtembelea hospitali ya Muhimbili alikolazwa, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi kwa tiketi ya Chadema,Mh.Joseph Haule maarufu kama Profesa J.

Joseph Haule aka Profesa Jay

Viongozi hao wa kitaifa wa Chama cha Mapinduzi leo wameamua kumtembelea mwanasiasa huyo wa upinzani baada ya kuwepo kwa taarifa za kulazwa kwake katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam yapata wiki ya tatu sasa!

Hii ni ishara kwamba Chama Cha Mapinduzi kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinaamini katika siasa zenye kujali umoja wa kitaifa,undugu,mshikamano,uhuru wa mawazo na ushiriki wa watanzania wote bila kujali Itikadi zao katika ujenzi wa Taifa!

Chama cha Mapinduzi kupitia Serikali yake ya AWAMU ya SITA kinedhamiria kwa dhati kabisa kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano bila kujali Itikadi ya mtu ya siasa au chama chake!

CCM imedhamiria tangu kuanzishwa kwake kuwa Chama Mama na mlezi wa vyama vingine ndani na nje ya Nchi katika kudumisha malengo ya makuu ya mwasisi wa Taifa la Tanzania,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri wa zamani,Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %