0 0
Read Time:48 Second

CHATO

WU®

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina amefanya ziara ya siku moja Wilayani Chato yenye lengo la kutoa salamu za pole kwa familia ya hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Akiwa nyumbani kwa hayati Dkt. John Pombe Magufuli Dkt. Akinwumi Adesina amesema amefika nyumbani kwa hayati Magufuli kutokana na urafiki mkubwa aliokuwa nao yeye na hayati Rais Magufuli pamoja na kutambua mchango mkubwa ambao hayati Magufuli aliutoa kwa watanzania na kwa watu wengine.

“Rais Magufuli alikuwa mfano mzuri kwa viongozi barani Afrika, aliwapenda watanzania na waafrika wote kwa moyo wake wote” alisema Dkt. Adesina.

Picha ya kumbukumbu wakati Rais wa AfdB alipo mtembelea Hayati Dr John Pombe Magufuli ikulu

Rais wa AfDB amesema pamoja na kuodokewa na Rais Magufuli anafarijika kuona Tanzania bado ipo kwenye mikono salama chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaendeleza yale yote mazuri yaliyoachwa na hayati Magufuli.

Dkt. Akinwumi Adesina amemshukuru Rais Samia kwa ushirikiano na kumruhusu kufika Wilayani Chato.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %