
WU®
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
February 13,2022.
Ni kama inataka kuwa kawaida kwa matukio ya kuungua kwa masoko Nchini kwa takribani ndani ya miezi sita tu tukianzia na soko kuu la Kariakoo,soko la karume na sasa soko la Mbagala, matukio yote yakitokea katika Jiji la Dar es salaam!
Kabla wananchi hawajapata repoti ya sababu za kuungua soko la Kariakoo,karume leo tena tunasikia tukio lingine la kuungua kwa soko la Mbagala, Mkoani Dar es salaam!
Je,kuna watu wapo nyuma ya mpango huu?je,dhamira zao ni zipi?wanatumwa na nani?na je,Khali hii itaendelea mpaka lini?soko lipi linafwata?,je,ni soko la Mwanjelwa jijini Mbeya,ni soko kuu la Chief Kingaru mkoani Morogoro au ni soko kuu la jijini Dodoma?
Chanzo kikuu cha moto huu ndani ya masoko yetu nchini kinadharia”anticipation” zinaweza kuainishwa katika makundi matatu ambayo ni;
1.Sababu za matishio ya kigaidi ambapo inawezekana matukio haya ya moto katika masoko yetu ni mipango ya siri inayoratibiwa na kikundi cha watu fulani fulani kwa lengo la kutimiza maslahi yao fulani fulani!
Kama sababu ni hii, ni kwamba, ugaidi una tabia ya kutaka kuonyesha uwepo wao katika eneo fulani lakini zaidi wanataka kuwaogopesha watu kuwa wao ni zaidi ya Serikali zetu na wanaweza kufanya tukio lolote na wasikamatwe!
Kitendo cha kutokea matukio matatu yanayofanana katika Mkoa mmoja kinanipa ishara ya kuwa uenda matukio haya yana viashiria vya kigaidi!
Tunaviachia vyombo vyetu vifanye kazi zao!
2.Sababu ya pili inaweza kuwa matukio haya yanatokea kwa sababu za kiuzembe katika mifumo yetu ya uthibiti majanga ya moto katika maeneo ya masoko yetu!
Je,ni wapi kuna tangazo sokoni la angalau kuvuta sigara ndani ya soko?angalau bango la usivute sigara!Je,mifumo yetu ya umeme katika masoko yetu ipoje?Tuanzie kuwaza hapo na tuwaze zaidi ya box!
3.Je,moto huu ni ishara ya HUJUMA?”Sabotage”!je,Nini kinatokea mpaka kunakuwepo na sabotage kama hizi?,je,ni migongano ya kimaslahi baina ya wadau katika masoko haya na kupelekea kufanya HUJUMA hizi?
Je,washiriki wa HUJUMA hizi ni mtu mmoja au kikundi cha watu?je,nini kinawasukuma kufanya HUJUMA hizi za kuchoma moto?
Tume yoyote itakayoundwa katika kutafuta chanzo cha moto katika masoko yetu lazima “zitambae” katika “Hypothesis” hizi tatu kujua ukweli wa matukio haya!Tunahitaji kuthibiti hali haraka kabla matukio haya hayajaacha umasikini mkubwa kwa wafanyabiashara wetu Nchini!
MASWALI MAGUMU YA KUJIULIZA KUHUSU MOTO MASOKONI NA MASHULENI NCHINI!
I.Kama matukio haya ni ya matukio ya kigaidi au HUJUMA,je,tuna shida katika mifumo yetu ya kupata taarifa”ability to detect before” matukio yenyewe kutokea hasa kwa matukio ambayo yanajirudia rudia?
II.Je,tuna matishio ya kigaidi ndani ya Nchi?kama ni ndio je,tunatokaje hapa tulipo?Matukio kama haya ya moto na milipuko pia mwaka jana yametokea katika Jiji la Kampala Uganda na baadhi ya watu kutangaza kwamba alikuwa nyuma ya mpango huo!
III.Je,kuna udhaifu katika mifumo yetu ya ulinzi wa masoko makubwa Nchini?Kwanini masoko yetu yasitumie walinzi angalau wenye viwango fulani vya elimu ya ulinzi?je,tunawatumiaje Suma JKT katika kulinda masoko yetu?ni masoko mangapi yanatumia Suma JKT Nchini?
IV.Je,kwanini target za majanga ya moto Nchini yawe katika Bar,Masoko na Shule?,kwanini isiwe Banki au Supermarket kubwa?,je,wafanya HUJUMA hizi wanatumia udhaifu wa ulinzi katika maeneo haya kufanya HUJUMA zao?
V.Je,zile taarifa za kitelijensia za kuwepo kwa mipango wa kulipua masoko na vituo vya mafuta Nchini bado unaendelea?je,taarifa zile ndio matokeo ya matukio haya?
Spidi hii ya majanga ya moto inaweza kuendelea katika masoko mengine kama sababu ni “sabotage”lakini zaidi kuna uwezekano watekelezaji wa matukio haya wakabadili “target areas”zao na kutekeleza mipango yao katika style nyingine, hili kutimiza kitu kinachoitwa “DISLOCATION”.
Kuvifanya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikose “concentration” katika kujua sababu za matukio haya!
+255746726484.








