WU®
Balozi Edwin Rutageruka Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi amefariki usiku huu wa leo saa moja katika Hospitali ya Aga Khan Dar Es Salaam ambako alikuwa amelazwa tokea jana jioni kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla. Tumuombee Balozi Edwin Rutageruka kwa Mwenyezi Mungu ajaliwe pumziko la amani na pia tumuombe Mwenyezi Mungu awafariji familia, ndugu, marafiki nasi watumishi wenzake kwenye kipindi hiki cha huzuni kubwa. Amen.