0 0
Read Time:2 Minute, 41 Second

Na Dr Yahya Msangi

LOME TOGO

Nimefuatilia mjadala kuhusu Bei ya mbolea na agizo la Waziri kuwa warejeshewe kilichozidishwa na wafanyabiashara wa mbole. Ni kichekesho cha Ukraine!

Inashangaza Waziri anasifiwa!

Kwanza inastaajabisha kwamba bei ya mbolea (nitrogen fertilizers – sulphate of ammonia na urea) ni Karibu Mara 2.5 ya bei ndani ya jumuia ya ulaya. Nasema inastaajabisha kwa kuwa kwa kiasi kikubwa malighafi ya kutengeneza mbolea tunayo zaidi kuliko nchi nyingi ulaya. Tungetegemea bei yetu iwe pungufu.

Pili inashangaza pia japo tuna ng’ombe wengi (per capita) bado hatujaona umuhimu wa kuzalisha mbolea ya samadi kwa wingi. Bado tukiwaza mbolea tunafikiria kina SA, UREA, NPK pekee! Kuna nchi EU zinakaribia kufikia uwiano WA 50:50 Kati ya samadi na mbolea kutokea viwandani (industrial fertilizers). Hatujaweza bado kupanga mifugo ituzalishie mbolea. Bado kwetu tukiwaza mifugo tunaishia kufikiri nyama, maziwa na ngozi. Samadi ina sawa au kuzidi maziwa. Hâta wafugaji wetu hawajui kwamba ni wamiliki wa viwanda vya mbolea!

Kuhusu agizo la Waziri hebu tuwaze Pamoja hivi : Hivi wakulima wetu wanatunza risiti za manunuzi? Achilia mbali wakila je wéwé inatunza risiti ya vyote unavyonunua? Watalipwaje bila risiti za manunuzi? Hivi Waziri hajui wafanyabiashara ama hawawapi wakulima risiti ama wanawapa feki? Watalipwaje walichoibiwa? Na hebu Fikiria MKULIMA mfano kapunjwa elfu ishirini na alinunua mbolea wilayani au mkoani. Alipe nauli, chakula na pengine malazi kufuata elfu ishirini? Au gharama za kufuata alichoibiwa itajazia serikali ?

Tunapenda sana matumizi ya maagizo ya papo kwa papo! Na kwa kuwa watu weshazoeshwa wanadhani ndio uchapa kazi.

Nilianza kwa kusema tulibugia dhana ya PPP BILA kutafuna. Haya ndio Matokeo!

Bahati njema niliwahi kufanya utafiti EU kuhusu mpango unaitwa COMMON AGRICULTURE POLICY (CAP). Japo wao ndio waasisi wa PPP (Private Public Partnership) kwenye pembejeo hawajaacha PPP itambe. Wakulima wanalindwa na serikali! Mfano CAP ilitenga nchi 4 ambazo mkulima alipaswa alindwe. hizo kwa utani zikiitwa “3rd World Countries of Europe”! Mkulima katika nchi Hizi hakuachwa apambane na nguvu ya Soko. Ukitizama walivyolindwa haina tofauti n’a jinsi Nyerere alivyowalinda wakulima Tanzania. Kulianzishwa TFA, TFC, Vyama vyao ushirika Ili kuwahamishia kupata pembejeo bila kupitia sokoni. Ikaja dhana ya PPA tukaua Hizi Kinga badala ya kuziboresha. Yakaanzishwa madudu sijui hati ghalani, mfuko wa pembejeo ambao wajanja ndiyo wanaufikia! Wabunge wetu wakawa ndio eneo lao la kujidai. Wakashiriki kuwaibia wakulima huku wakizuga wanawawakilisha! Ukifanyika uchunguzi itabainika ni kina nani walinufaika na hati ghalani na mfuko wa pembejeo. Hawa ndio walikuwa almaarufu kwa kusambaza mbolea n’a mbegu hafifu. Popote duniani ambapo dhana ya PPA ilibugiwa bila kutafuna haya madudu hayakwepeki. Ndio maana baadhi yetu tafsiri sahihi ya PPA = POOR PEOPLE’S ANTHRAX.

Ushauri: tuongeze uzalishaji mbolea za kiwandani na samadi. Mbali ya nyama, maziwa na ngozi tuongeze samadi kama malengo makuu ya sekta. Tuwalinde wakulima kwa kuwaondosha wafanyabiashara kwenye pembejeo. Tufufue kina TFC, TFA na vyama vya wakulima. Tuwakabidhi wakulima waviendeshe na serikali isimamie tu. Isiwateulie wakulima watendaji.

Na mwisho Tuache kutolea maamuzi ya kutafuta sifa kwenye masuala nyeti. Waziri kabla hujakurupuka kutoa maagizo ongea na wataalamu. Haya maagizo ya papo kwa papo Ili tu kufurahisha watu hayatatufikisha tunakotaka kwenda. Mfano: unaonaje ungeagiza warejeshe walichoibiwa wakulima wizarani halafu wizara ndio iwapelekee wakulima? Ungegundua wakulima wengi hawana risiti au walizonazo hazionyesho waliibiwa.

Na huu mtindo wa mwizi aliyekiri kaiba anaagizwa arejeshe yaishie hapo ni vipi?

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %