0 0
Read Time:3 Minute, 24 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
March 19,2021.

Siku kama ya leo mwaka jana 202, Mwanamama mmoja mtulivu kutoka visiwa vya Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaandika historia yake binafsi na historia ya Taifa la Tanzania kwa kumpata RAIS wa kwanza Mwanamama, Mh.Samia Suluhu Hassan!

Pamoja na kutokuwa na maandalizi ya kubeba dhamana hii kubwa lakini Mh.Samia Suluhu Hassan, amethibitisha pasipo shaka kuwa kazi hii anaiweza kuliko wengi walivyodhani na hapa namnukuu!

“…walinitazama na kuniweka katika grade zao …sasa wanashangaa kuwa ni huyu tuliyompa grade ileee.?..,najua ni homa ya 2025 tu…”!

Wakati Mh.Rais ametimiza mwaka mmoja wa kuwa madarakani leo,kwangu mimi hizi ni alama tano ambazo haziwezi kufutika mioyoni mwa watanzania;

I.KUPANDISHA VYEO WATUMISHI WA UMMA!

Vyombo vya ulinzi na usalama ndivyo ambavyo naweza kusema vimekula bata sana ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu hassan!Mwaka mmoja ulikuwa wa neema sana kwa askari na makamanda wa jeshi la Magereza,Polisi,Uhamiaji,zimamoto!

Askari na makamanda kutoka vyombo hivyo ambao walikuwa wamesimama kupanda vyeo kwa takribani miaka MITANO ya JPM angalau mabega yao sasa yalianza kuvimba!

Jamaa ZANGU wa majeshi wanajua ninachosema hapa!Waulize watakwambia nini maana ya mwaka mmoja wa Mama Samia Suluhu Hassan kwao!

II.AJIRA NDANI YA SERIKALI NA NJE YA SERIKALI ZIMEKUWA ZA KUMWAGA SASA!

Kama kuna mtu anabisha kwamba mwaka mmoja wa Mama Samia hassan haukuwa ni mwaka wa kufungua ajira na aseme hapa!Kwa mara ya kwanza majeshi ya Magereza,Polisi,zimamoto na vyombo vingine vya ulinzi na usalama viliweza kutangaza ajira zaidi ya 700 kwa mpigo!

Hii ina maana kuwa zaidi ya vijana wa kitanzania 700 wameweza kuajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama ndani ya mwaka mmoja na hii haijawahi kutokea tangia uhuru!Ni mama Pekee yake ndio kaweza kuweka rekodi hii ya kibabe ndani ya mwaka wake mmoja tu madarakani!

III.KUSAINIWA KWA MIRADI MIKUBWA MITATU YA MADINI “KIBABE”.

Ndani ya mwaka mmoja wa Mama Samia ameweza kutoa leseni tatu kubwa za uchimbaji wa MADINI Nchini na kuifanya serikali yake kuwa na uhakika wa kutengeneza mapato ya serikali pamoja na ajira za moja kwa moja kwa watanzania si chini ya 3000 pindi miradi migodi hiyo itakapoanza kuzalisha hivi karibuni!

Unajua hii ina maana gani?sekta ya biashara na ujasiliamali inategemewa kukua kwani mahitaji ya migodi uendana na ujenzi wa makazi ya wafanyakazi wa mgodini,vyakula,mavazi na huduma za afya katika maeneo husika!Huu kwangu ni ushindi mkubwa ndani ya mwaka mmoja tu wa kibabe wa Samia Suluhu Hassan!Hii ni show ya kibabe ya Mama!

IV.WANAWAKE NA UONGOZI WA TAIFA!

Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kuiweka Tanzania katika ramani ya Dunia kuhusu wanawake na uongozi wa KITAIFA!Ndani ya mwaka mmoja wa Samia Suluhu Hassan,dunia imeweza kushuhudia mambo makubwa mawili kutokea Tanzania!

Moja ni uteuzi wa Spika wa pili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tokea uhuru Dk Tulia Ackson Mwansasu na pili ni uteuzi wa waziri wa ulinzi wa kwanza mwanamke tangia uhuru wa Taifa hili,Mama Sigomenda Tax!

Tanzania na hasa Rais Samia hassan anaingia katika rekodi za kimataifa kwa kuweza kuteua wanawake wengi hasa katika nafasi nyeti za uongozi ndani ya Taifa ndani ya mwaka mmoja tu!

V.KUPANDA KWA TAKWIMU ZA UWEKEZAJI KUTOKA NJE KUJA NDANI YA TZ!

Ndani ya mwaka mmoja tu TIC imeweza kuja na takwimu za kutisha za kibabe kuhusu UWEKEZAJI kutoka Nje,!Hii ni show show KWELI KWELI!

Mfano,wakati mradi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda -Tanga ukitaka kukwama,Rais Samia alikwea pipa na kwenda Uganda kwenda kuweka sawa baadhi ya mikwamo na mpaka sasa mradi wa Hoima Uganda -Tanga unatazamiwa kuanza wakati wowote ule!Hii ni ndani ya mwaka wake mmoja tu!

Mikataba minono ya UWEKEZAJI kutoka Nje tayari imeshasainiwa katika Nchi za ufaransa,Ubeligiji,Dubai na kwingineko hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa Nchi chache barani afrika zinazoangaliwa sana kwa sasa na wawekezaji duniani!

Mwaka mmoja,siku 365 za kibabe za Mh. Samia Suluhu Hassan pale Ikulu ya Chamwino Dodoma kamwe haziwezi kufutika kirahisi ndani ya Akili na MIOYO ya Watanzania!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %