0 0
Read Time:2 Minute, 10 Second

WU® Media PRODUCTION

Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia wamefanya ziara Rasmi ya kumtembelea Mstahiki Meya (Mayor) Mhe. Ruggero Mucchi, Meya wa Mji wa Cles Kaskazini mwa nchi ya Italia.

Bendera ya Tanzania ikipepea Rasmi katika Makao Makuu ya Manispaa ya Cles kufuatia Ugeni Rasmi wa Tanzania katika Mji huo wa Cles Kaskazini mwa Italia.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo alipokea mwaliko rasmi kufuatia Mkataba wa Mashirikiano uliosainiwa Mwaka 2018 kati ya Meya huyo wa Manispaa ya Cles, Wilaya ya Trento, na Manispaa ya Wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba.

Mkataba huo uliotiwa saini na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya ChakeChake wakati huo ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadid Rashid, na kukubaliana masuala kadhaa ya mashirikiano ambayo Ubalozi wa Tanzania nchini Italia umekubali jukumu la kuratibu na kufuatilia kwa Karibu makubaliano hayo. Miongoni mwa makubaliano na mashirikiano hayo ni pamoja na Maabara ya PHL iliyopo Vitongoji katika Wilaya ya Chake Chake Pemba, ambayo inasimamiwa kwa mashirikiano na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Ivo di Carneri Foundation chini ya usimamizi wa Bi. Sandra Carrozi na Wizara ya Afya Zanzibar.

Kutoka Kushoto ni Rais wa Ivo di Carneri Mama Sandra Carrozi Carneri, Mstahiki Meya wa Mji wa Cles Mhe. Ruggero Mucchi, BALOZI wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ivo di Carneri anayefanyia kazi zake Kisiwani Pemba katika Maabara ya Chake Chake Kisiwani Pemba, na Balozi wa Heshima nchini Italia Prof. Marco Conca wakiwa mbele ya Jengo na Makao Makuu ya Mji wa Cles huku Bendera ya Tanzania ikipeperushwa rasmi kutokana na Ugeni huo.
Mstahiki Meya wa Mji wa Cles Mhe. Ruggero Mucchi akiwa na BALOZI wa Tanzania nchini Italia katika Afisi ya Mstahiki Meya alipofanya ziara Rasmi katika Mji huo kwa mwaliko wa Mstahiki Meya huyo ambaye alitiliana Saini Mkataba wa Mashirikiano na Miji Pacha mnamo Mwaka 2018 na Wilaya na Manispaa ya Chake Chake, Pemba nchini Tanzania.
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia wakiwa pamoja na Mama Sandra Carozzi, Rais wa Taasisi ya Ivo di Carneri ya nchini Italia ambayo inafanyia kazi zake Kisiwani Pemba katika Maabara ya ChakeChake juu ya kupambana na maradhi ya Kichocho.
Mhe. Mstahiki Meya wa Mji wa Cles Kaskazini mwa Italy Bw. Ruggero Mucchi akiwa na Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Italia Mahmoud Kombo na Maafisa wa Ubalozi Eva Kaluwa na Sigifred Nnembuka, Balozi wa Heshima wa Tanzania Prof. Marco Conca na Rais wa Jumuiya ya Mji na Bonde la Cles, kukamilisha mazungumzo ya mashirikiano ya Usafi wa Mazingira kwa Tanzania.
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %